Posts

Showing posts from December, 2021

ZAIDI YA MILIONI 90 KUWANUFAISHA WAJASILIAMARI RUKWA

Image
 RC MKIRIKITI: MIKOPO YA HALMASHAURI ITUMIKE KUKUZA UCHUMI Vijana,Wanawake na watu wenye ulemavu wametakiwa kutumia mikopo ya fedha Vifaa walivyopatiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kukuza uchumi wa kaya na kuzalisha ajira miongoni mwa wanufaika. Hayo yamebainishwa leo (31.12.2021) na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti wakati wa hafla  ya kukabidhi mikopo ya bajaji, bodaboda na fedha kwa wajasiliamali  iliyofanyika katika viwanja vya bustani ya Mandela mjini Sumbawanga. " Ni vizuri mkatumie fedha hizi kwa lengo la kukuza ajira na kipato cha kaya zenu na Taifa  kwani serikali inatoa fedha hizi kama mkopo na mtakaporejesha basi vijana na akina mama wengine watanufaika nayo" alisisitiza Mkirikiti Aidha amewapongeza wanufaika kwa kurejesha mikopo yao yote ya awamu ya kwanza bila usumbufu na ameagiza kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoa elimu  zaidi ili wananchi wajue namna ya kupata mikopo na kuweza kujikimu. Katika hafla ya leo Manispaa ya Sumbawanga...

RC MKIRIKITI WAKULIMA TUZINGATIE HAYA

Image
 Na: Franco NKYANDWALE  Sumbawanga.  RC RUKWA:  LIMA MAZAO YANAYOSTAHIMILI UKAME. Wakulima wa mkoani Rukwa wameshauriwa kulima mazao yanayostahimili ukame kutokana na mwenendo wa unyeshaji wa mvua mwaka huu ambao si wa kuridhisha. Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti alitoa rai hiyo mwishoni mwa mwezi Disemba, 2021 mjini Sumbawanga wakati akizungumza kwenye kikao cha kusimamia, kuratibu na kudhibiti mapato na matumizi ya serikali robo ya pili kilichohudhuriwa na wakurugenzi wa halmashauri zote mkoani Rukwa. *“Mvua zimechelewa sana. Katika wilaya zetu tumeshuhudia kiwango kidogo cha mvua hadi sasa, hivyo ni wakati muafaka wataalamu wa kilimo wakaelimisha wakulima kupanda mazao yanayostahimili ukame “* alisisitiza Mkirikiti kwa kusema kuwa serikali imechukua hatua kadhaa ikiwemo kugawa mbegu za soya na alizeti ili wakulima wazalishe mazao hayo ambayo hayaihitaji mvua nyingi na kwamba jitihada zaidi zinatakiwa kutumia kilimo cha umwagiliaji katika mabonde yaliyopo ili...

WAZIRI WA MAJI AAGIZA HAYA KWA MSISITIZO

Image
  Na Peter Helatano W aziri wa Wizara ya Maji Jumaa Aweso amewaagiza Meneja wote wa Wakala wa Maji vijijini RUWASA kutumia maadhimisho ya Wiki ya Maji Duniani kwaajili ya kujenga na kuzindua miradi ya maji kwenye maeneo ambayo wananchi bado wanatabika na kero ya maji. Waziri Aweso aliyasema hayo jana wakati alipokutana na kuzungumza na watumishi wa sekta ya maji pamoja na viongozi wengine mkoani Rukwa. Awes o alisema haina maana serikali kutoa fedha kwaajili ya uje n z i wa miradi ya maji lakini fedha hizo zimekuwa zikakaa pasipo kutumika huku wananchi wakiendelea kuteseka kusaka maji umbali mrefu. Waziri Aweso amewaagiza Mameneja wa wakala wa Maji vijijini wote kila ifikapo Machi 22, Kutumia siku hiyo kwaajili ya uzinduzi wa Miradi ya maji ili ku wapunguzia wanachi kero Waziri Aweso Katika   ziara ya Ukaguzi na Uzinduzi wa Miradi ya Maji Mkoani Rukwa Ambapo pia ame wapongeza RUWASA Kwa KAZI nzuri wanayofanya Mkoani Ruk wa .

UZINDUZI WA MNARA WA MIAKA 60 YA UHURU

Image
 UZINDUZI WA MNARA WA KUMBUKUMBU YA MIAKA 60 YA UHURU SUMBAWANGA  Katika kuadhimisha sherehe za uhuru wa Tanzania Bara leo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti akiwa na Wazee wa Mji wa Sumbawanga wamezindua jiwe la msingi la mnara wa kumbukumbu ya miaka 60 ya uhuru mahala ambapo bendera ya Tanganyika huru ilipandishwa mara ya kwanza Desemba 09 ,1961. Tukio hilo limefanyika leo eneo la Bomani wikaya ya Sumbawanga  ambapo Mkuu huyo wa Mkoa akiwa na wazee ambao walikuwepo siku ya uhuru mwaka 1961 . Eneo hilo lililopo jirani na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga  patajengwa mnara huo mapema mwaka huu ili iwe ni kumbukumbu muhimu kwa vizazi vijavyo.

MIAKA 60 YA UHURU..MKOA WA RUKWA...PICHA

Image
 Matukio Katika PICHA:Uzinduzi wa mnala wa kumbukumbu ya MIAKA 60 ya UHURU..Mkoani Rukwa Published by Peter Helatano

TUONGEZE JITIHADA..MIAKA 60 YA UHURU

Image
 RC MKIRIKITI: MIAKA 60 YA UHURU IFANYE WATUMISHI WA UMMA KUSHIKAMANA Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti amewataka watumishi wa umma kutumia sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara kuendeleza amani na mshikamano mahala pa kazi. Ametoa wito huo leo (08.12.2021) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru ambapo amewapongeza kwa kazi nzuri iliyochangia maendeleo ya taifa. " Nimekuja hapa kuwapongeza watumishi wote wa Manispaa kwa niaba ya watumishi wengine wa umma wa mkoa wa Rukwa kwa kazi nzuri mliyofanya hata leo Taifa letu linafikia mafanikio ya miaka 60 ya kuwa huru. Endeleeni kuwa wazalendo kwa taifa letu " alisema Mkirikiti. Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na Mkuu wa Wilaya Sebastian Waryuba na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Jacob Mtalitinya watumishi wametakiwa kuendelea kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia haki,upendo na mshikamano . Mkirikiti alitumia fursa hiyo k...

CHUKUENI MAAMUZI..RC MKIRIKITI

Image
  Na Franco NKYANDWALE NKASI  "Chukua maamuzi sasa ya kuchanja ili ujiepushe na ugonjwa wa CORONA ambao huua watu kwa uharaka.  CORONA inaendelea kuangamiza watu kote duniani na wala si mchezo chukua TAHADHARI.  Tuchanje  ili kujikinga na gojwa la CORONA ambapo serikali ya TANZANIA inatoa chanjo bure kwa watu wote”  Asema huko NKASI, Mkuu wa Mkoa RUKWA Joseph Joseph Mkirikiti. Published by Peter Helatano

HII MIRADI HAINA SIASA..TUFANYE KAZI

Image
Na Peter Helatano  Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti leo amefanya ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa madarasa ambapo ameagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Lightness Msemo kuongeza kasi ya usimamizi pamoja na kuongeza idadi ya mafundi ili spidi ya kazi iwe kasi. Mkuu wa mkoa amewasihi kujitahidi kufanya kazi ikiwezekana usiku na mchana ili kuhakikisha wanaenda na kasi ya Tarehe iliyowekwa kukamilisha ujenzi wa Vyumba vya madarasa ili kusiwe na shida ya madarasa kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na kidato Cha Kwanza. Aidha amewataka madiwani kuwa na ushirikiano kusimamia MIRADI na sio kuikwamisha kwa namna moja au nyingine, ''Miradi hi ya ujenzi wa Vyumba vya madarasa haina siasa tufanye kazi kwa kujituma''Alisema MKIRIKITI. Aidha ameagiza vituo vya Afya ambavyo vilishapatiwa fedha wataalam watafutwe na ukarabati uendelee Mara moja hii ni baada ya kupokea malamiko kutoka kwa wananchi wa Mtowisa ambao walilamikia kukosa huduma za Afya Katika eneo lao Huku fed...

RAIS SAMIA AKIWA NA KITUKUU WA HAYATI BABA WA TAIFA

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Kitukuu cha Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wakati alipomtembelea Mama Maria Nyerere kumjulia hali nyumbani kwake Msasani  Jijini Dar es Salaam leo tarehe 05 Desemba, 2021.

FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

Image
 Published by Peter Helatano. Afisa Mipango Miji wa Jiji la Dodoma, Aisha Masanja akielezea fursa za uwekezaji zilizopo katika Jiji la Dodoma kwenye Mkutano wa mwaka wa Shirikisho la wenye viwanda Tanzania (CTI) uliofanyika katika Hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam. Katikati ni kiongozi wa timu ya kimkakati ya Uwekezaji na Masoko ya Jiji la Dodoma, Leonard Machunde na kulia ni Mchumi Mwandamizi katika Jiji la Dodoma, Abeid Msangi wakifuatilia kwa umakini mkubwa hali ya mambo katika wasilisho hilo. AGM CTI Na. Dennis Gondwe, DAR ES SALAAM WAWEKEZAJI wenye viwanda nchini wamealikwa kuwekeza katika ujenzi wa viwanda katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma ili kuchangia katika ukuzaji wa uchumi na ujenzi wa makao makuu ya nchi.Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mipango Miji katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Aisha Masanja alipokuwa akiwasilisha fursa za uwekezaji zilizopo katika Jiji hilo kwenye Mkutano wa Mwaka wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI) uliofanyika katika hoteli ya P...

SIKU YA UKIMWI DUNIANI..VIONGOZI MKOA WA RUKWA

Image