WAZIRI WA MAJI AAGIZA HAYA KWA MSISITIZO



 Na Peter Helatano

Waziri wa Wizara ya Maji Jumaa Aweso amewaagiza Meneja wote wa Wakala wa Maji vijijini RUWASA kutumia maadhimisho ya Wiki ya Maji Duniani kwaajili ya kujenga na kuzindua miradi ya maji kwenye maeneo ambayo wananchi bado wanatabika na kero ya maji.

Waziri Aweso aliyasema hayo jana wakati alipokutana na kuzungumza na watumishi wa sekta ya maji pamoja na viongozi wengine mkoani Rukwa.

Aweso alisema haina maana serikali kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa miradi ya maji lakini fedha hizo zimekuwa zikakaa pasipo kutumika huku wananchi wakiendelea kuteseka kusaka maji umbali mrefu.

Waziri Aweso amewaagiza Mameneja wa wakala wa Maji vijijini wote kila ifikapo Machi 22, Kutumia siku hiyo kwaajili ya uzinduzi wa Miradi ya maji ili kuwapunguzia wanachi kero

Waziri Aweso Katika ziara ya Ukaguzi na Uzinduzi wa Miradi ya Maji Mkoani Rukwa Ambapo pia amewapongeza RUWASA Kwa KAZI nzuri wanayofanya Mkoani Rukwa.


Comments

Popular posts from this blog

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MAENDELEO YA CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA