ZAIDI YA MILIONI 90 KUWANUFAISHA WAJASILIAMARI RUKWA


 RC MKIRIKITI: MIKOPO YA HALMASHAURI ITUMIKE KUKUZA UCHUMI

Vijana,Wanawake na watu wenye ulemavu wametakiwa kutumia mikopo ya fedha Vifaa walivyopatiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kukuza uchumi wa kaya na kuzalisha ajira miongoni mwa wanufaika.


Hayo yamebainishwa leo (31.12.2021) na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti wakati wa hafla  ya kukabidhi mikopo ya bajaji, bodaboda na fedha kwa wajasiliamali  iliyofanyika katika viwanja vya bustani ya Mandela mjini Sumbawanga.


" Ni vizuri mkatumie fedha hizi kwa lengo la kukuza ajira na kipato cha kaya zenu na Taifa  kwani serikali inatoa fedha hizi kama mkopo na mtakaporejesha basi vijana na akina mama wengine watanufaika nayo" alisisitiza Mkirikiti


Aidha amewapongeza wanufaika kwa kurejesha mikopo yao yote ya awamu ya kwanza bila usumbufu na ameagiza kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoa elimu  zaidi ili wananchi wajue namna ya kupata mikopo na kuweza kujikimu.


Katika hafla ya leo Manispaa ya Sumbawanga imetoa mikopo isiyo na riba yenye jumla ya shilingi Milioni 118.5 .


Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Sumbawanga Frank Mateni amesema mikopo hiyo ambayo jumla yake inafikia shilingi Milioni 118.5 imetolewa ikiwa ni utekelezaji wa bajeti ya serikali na mkakati wa kuwezesha wananchi kiuchumi kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri.

Published by Peter Helatano

Comments

Popular posts from this blog

Watumishi Wa Umma Wilayani Kalambo Waungana Kuadhimisha Kumbukizi Ya Mashujaa Kwa Kufanya Usafi.

Dc Kalambo Ataka Walio Husika Kumuozesha Mwanafunzi Wa Darasa La Saba Kukamatwa

Mkurugenzi UTPC awataka Waandishi kuandika Habari za Usawa wa kijinsia ili kuleta mabadiliko Chanya katika jamii.