Na Baraka Lusajo - Rukwa. Vyama vya Ushirika wilayani Kalambo mkoani Rukwa vimetakiwa kuwekeza nguvu zao katika upatikanaji wa zana bora za kilimo ili kuweza kuongeza uzalishaji na ubora wa mazao mbalimbali mkoani Rukwa hasa katika kipindi hiki wanachojiandaa kuanza msimu mpya wa kilimo unaotarajiwa kuanza mwezi Oktoba mwaka huu. Akiongea wakati wa Ufunguzi wa uzinduzi wa Mkakati wa matumizi bora ya zana za kilimo, Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Rukwa, Ocran Chengula alisema kuwa, asilimia 80 ya uchumi wa Mkoa wa Rukwa unategemea kilimo lakini ni asilimia 3 tu ya wakulima wanatumia matrekta hali inayopekelea eneo kubwa la ardhi inayofaa kulimwa katika mkoa huo kutolimwa na pia kutopata mazao bora yenye kuhimili ushindani katika soko la dunia. “Katika mkoa wetu kuna hekta 1,660,000 ambazo zinafaa kwa kilimo, lakini kati ya hizo kwa kiasi kikubwa sana tunazoloma ni hekta laki tano na kidogo, ambazo ni sawa na asilimia 32 kuna kipi...
Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Deogratius Nsokolo amesema ili kusaidia kupunguza hali ya uhasama dhidi ya Waandishi wa Habari UTPC inaendelea kutumia Klabu za Waandishi wa Habari mikoani kuhamasisha na kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa Uhuru wa vyombo vya Habari na jukumu la Waandishi wa Habari katika jamii. Nsokolo ameyasema hayo Leo Novemba 2,2023 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa siku ya Kimataifa ya kukomesha Uhalifu dhidi ya Waandishi wa Habari ulioandaliwa na UTPC na kufanyika kwa njia ya mtandao(Zoom). Amesema maadhimisho hayo kwa mwaka 2023 yanalenga Kuongeza uelewa kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo Waandishi katika kutekeleza majukumu Yao,lakin pia kuonya juu ya kukithiri kwa vitendo vya kikatili na ukandamizaji dhidi ya Waandishi wa Habari. Aidha akiongelea kujenga Mazingira salama kwa Waandishi wa Habari amewashukuru ubalozi wa Uswiss hapa Nchini Tanzania,kwa ufadhili wao katika mradi na Mkuu wa jeshi la polisi Nchini IG...
CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA CHAFIKIA 64% KUJENGWA Na. OMM Rukwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imepongezwa kwa kuwezesha upatikanaji fedha shilingi 3,852,697,911 zinazotumika katika awamu ya kwanza kujenga majengo 11 ya chuo kipya cha Ualimu Sumbawanga eneo la Pito ambapo mradi huo umefikia asilimia 64 hadi sasa. Akizungumza leo (06. 07.2022) kwenye ukaguzi wa mradi huo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti aliwaeleza waandishi wa habari kuwa serikali inatekeleza mradi huo kwa lengo la kufungua fursa za kielimu kwa wananchi ambapo utakapokamilika utasidia kuchochea ukuaji wa uchumi. "Rukwa tumenufaika na mradi huu wenye thamani ya shilingi Bilioni 3.9 ambapo majengo kadhaa yamekamikika na mengine jitihada za ukamilishaji zinaendelea vizuri. Nimeridhishwa na kazi inayoendelea hapa na kuhusu changamoto chace nitawasiliana na Wizara ya Elimu tuzitatue mapema na mradi ufike mwisho" ,alisema Mkirikiti. Katika hatua nyingine Mkuuu huyo wa ...
Comments
Post a Comment