RC MKIRIKITI WAKULIMA TUZINGATIE HAYA



 Na: Franco NKYANDWALE  Sumbawanga. 

RC RUKWA: 

LIMA MAZAO YANAYOSTAHIMILI UKAME.

Wakulima wa mkoani Rukwa wameshauriwa kulima mazao yanayostahimili ukame kutokana na mwenendo wa unyeshaji wa mvua mwaka huu ambao si wa kuridhisha.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti alitoa rai hiyo mwishoni mwa mwezi Disemba, 2021 mjini Sumbawanga wakati akizungumza kwenye kikao cha kusimamia, kuratibu na kudhibiti mapato na matumizi ya serikali robo ya pili kilichohudhuriwa na wakurugenzi wa halmashauri zote mkoani Rukwa.


*“Mvua zimechelewa sana. Katika wilaya zetu tumeshuhudia kiwango kidogo cha mvua hadi sasa, hivyo ni wakati muafaka wataalamu wa kilimo wakaelimisha wakulima kupanda mazao yanayostahimili ukame “* alisisitiza Mkirikiti kwa kusema kuwa serikali imechukua hatua kadhaa ikiwemo kugawa mbegu za soya na alizeti ili wakulima wazalishe mazao hayo ambayo hayaihitaji mvua nyingi na kwamba jitihada zaidi zinatakiwa kutumia kilimo cha umwagiliaji katika mabonde yaliyopo ili kuwa na uhakika wa mazao ya chakula.


Aidha Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Denis Bandisa akizungumza kwenye kikao hicho aliwakumbusha viongozi wa halmashauri kuendelea kutenga fedha na kutekeleza afua za lishe ili kuondokana na tatizo la udumavu na utapiamlo kwa watoto chini ya miaka mitano.

Published by Peter Helatano from Android Phone

Comments

Popular posts from this blog

Watumishi Wa Umma Wilayani Kalambo Waungana Kuadhimisha Kumbukizi Ya Mashujaa Kwa Kufanya Usafi.

Dc Kalambo Ataka Walio Husika Kumuozesha Mwanafunzi Wa Darasa La Saba Kukamatwa

Mkurugenzi UTPC awataka Waandishi kuandika Habari za Usawa wa kijinsia ili kuleta mabadiliko Chanya katika jamii.