HII MIRADI HAINA SIASA..TUFANYE KAZI


Na Peter Helatano
 Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti leo amefanya ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa madarasa ambapo ameagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Lightness Msemo kuongeza kasi ya usimamizi pamoja na kuongeza idadi ya mafundi ili spidi ya kazi iwe kasi.
Mkuu wa mkoa amewasihi kujitahidi kufanya kazi ikiwezekana usiku na mchana ili kuhakikisha wanaenda na kasi ya Tarehe iliyowekwa kukamilisha ujenzi wa Vyumba vya madarasa ili kusiwe na shida ya madarasa kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na kidato Cha Kwanza.

Aidha amewataka madiwani kuwa na ushirikiano kusimamia MIRADI na sio kuikwamisha kwa namna moja au nyingine,
''Miradi hi ya ujenzi wa Vyumba vya madarasa haina siasa tufanye kazi kwa kujituma''Alisema MKIRIKITI.

Aidha ameagiza vituo vya Afya ambavyo vilishapatiwa fedha wataalam watafutwe na ukarabati uendelee Mara moja hii ni baada ya kupokea malamiko kutoka kwa wananchi wa Mtowisa ambao walilamikia kukosa huduma za Afya Katika eneo lao Huku fedha za ujenzi wa kituo Chao tayari zishatolewa na ujenzi hauendeleei fedha zimehifadhiwa tu.



Comments

Popular posts from this blog

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MAENDELEO YA CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA