WANANCHI WATAKIWA KUPANDA MITI KUTUNZA MAZINGIRA.
WANANCHI
WATAKIWA KUPANDA MITI KUTUNZA MAZINGIRA.
Wananchi
mkoani Rukwa wametakiwa kuacha tabia ya kukata miti ovyo na kufanya shughuli za
kilimo kwenye vyanzo vya maji
Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Rukwa Queen Sendiga alipotembelea ofisi ya klabu ya waandishi wa habari mkoani Rukwa na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi yao
Sendiga amesema anatarajia kupokea miche ya miti milioni moja ambayo tayari imeandaliwa na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Mkoa wa Rukwa na itapandwa kwenye kingo za barabara na kwenye vyanzo vya maji.
Aidha
amewataka watendaji wa kata na vijiji kwenye maeneo yao kuhakikisha wanasimamia
zoezi la upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira.
Katika hatua nyingine Sendiga amesema atahakikisha waandishi wa habari wanashirikiana na taasisi nyingine Katika kuutangaza Mkoa wa Rukwa na kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira.
Comments
Post a Comment