WATATU MBALONI UTAPELI KIMTANDAO
WATATU
MBALONI UTAPELI KIMTANDAO
Jeshi la
Polisi Mkoani Rukwa limewakamata wauhumiwa watatu(3)wanaume wakazi wa
Sumbawanga amabo wanaojihusisha na
uhalifu wa kimtandao kwa njia ya kupiga simu na kuwatishia watu kwa nia ya
kujipatia kipato.
Akitoa
taarifa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa
wa Rukwa ACP- Shadrack Masija amesema wimbi la utapeli kupitia mtandao Mkoani
Rukwa limekuwa likiongezeka na kusema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea
kujiimarisha na kuhakikisha wanatokomoeza utapeli wa kimtandao wa aina yotote
ili kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani na utulivu.
Aidha Katika
hatua nyingine Kamanda Masija amesema kumekuwepo na matukio mbalimbali ya watu
kupoteza maisha kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Katika Mkoa wa Rukwa
mabapo Katika Wilaya ya Nkasi kumetokea vifo vya watu wawili akiwemo mwanafunzi
mmoja na mvuvi mmoja,Wilaya ya kipolisi Laela kumetokea kifo cha mtu mmoja
aliyetumbukia kwenye dimbwi lililojaa maji baada ya mvua kubwa kunyesha na
kupelekea kifo chake.
Jeshi la
Polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kuota ushirikiano Katika kuripoti na
kuzuia vitendo vya uhalifu au vinavyoweza kuhatarisha amani.
Comments
Post a Comment