Waziri Bashe akiri Matumizi ya mbolea Mkoa wa Rukwa yameongezeka

 


*Waziri Bashe akiri Matumizi ya mbolea Mkoa wa Rukwa yameongezeka* 

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameeleza kuwa, matumizi ya mbolea kwa mkoa wa Rukwa msimu huu wa kilimo(2022/2023) yameongezeka tofauti na msimu wa kilimo 2021/2022.

Alisema,  matumizi ya mbolea kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kwa msimu wa kilimo 2021 ilikuwa ni tani 1600 lakini msimu wa kilimo 2022/2023 kuanzia  tarehe 15 Agosti, 2022  mpaka tarehe 3 Januari 2023 kiasi cha tani 842 sawa na asilimia 50 ya mbolea zilizotumika msimu uliopita wa kilimo kimetumika. 

Amebainisha matumizi  ya mbolea kwa msimu uliipita yanalingana na matumizi ya mbolea kwa nusu msimu wa mwaka 2022/23 japo msimu wa kilimo bado unaendelea na kubainisha muitikio wa matumizi ya mbolea umekuwa mkubwa kutokana na bei za mbolea kushuka pamoja na kupanda kwa bei ya nafaka kulikowafanya wakulima kuongeza mashamba  yao ya kulima.

Waziri Bashe amebainisha hayo jana tarehe 4 Januari, 2023 alipokuwa katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya siku mbili mkoani Rukwa kilichohuhusisha watendaji wa Serikali na Chama Wafanyabiashara wa mbolea, waingizaji na wasambazaji wa mbolea pamoja na wananchi.

Akitoa taarifa ya mauzo ya kiasi cha mbolea kilichouzwa kwa msimu uliopita wa kilimo, Waziri Bashe alisema, msimu wa 2021 waliuza Tani 1120 na mpaka tarehe 3 Januari 2023 wameuza kiasi cha   tani 4000 kwa kampuni la OCP wakati ETG kwa msimu wa 2021 waliuza tani 1700 mpaka tarehe 03 Januari, 2023 kiasi cha tani 17000 za mbolea zimeuzwa.

"Ningekuta kiasi cha mbolea kilichofika Nkasi ni kidogo kuliko msimu uliopita ningejua kuna crisis lakini kwa hali ilivyo bado tupo katika nafasi nzuri na uzuri usambazaji wa mbolea unaendelea" Waziri Bashe alisisitiza.

Alisema, katika kutatua changamoto ya upatikanaji wa mbolea karibu na maeneo ya wakulima Mamlaka ya Serikali ya Mkoa itateua vituo tutakavyosajiliwa ili kuwawezesha mawakala kufikisha mbolea katika maeneo hayo kwani mbolea haiwezi kuuzwa  katika vituo ambavyo havijasajiliwa.

Aliongeza kuwa, wamekubaliana na makampuni kuhakikisha wanapeleka mbolea karibu na wakulima na kubainisha atawafutia leseni endapo hawatafuata maelekezo  aliyoyatoa wakati wa ziara hiyo.

Aidha, alilishukuru kqmpuni la usambazaji wa mbolea la ETG kwa  kuitika wito baada ya maelekezo aliyotoa ambapo tayari wamepeleka na kuanza kuuza mbolea katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi.

Comments

Popular posts from this blog

Watumishi Wa Umma Wilayani Kalambo Waungana Kuadhimisha Kumbukizi Ya Mashujaa Kwa Kufanya Usafi.

Dc Kalambo Ataka Walio Husika Kumuozesha Mwanafunzi Wa Darasa La Saba Kukamatwa

Mkurugenzi UTPC awataka Waandishi kuandika Habari za Usawa wa kijinsia ili kuleta mabadiliko Chanya katika jamii.