SERIKALI KUWEKA NGUVU ZAIDI UTUNZAJI WA MAZINGIRA


 

SERIKALI KUWEKA NGUVU ZAIDI UTUNZAJI WA MAZINGIRA

Na Peter Helatano-Rukwa

Katika miaka kadhaa suala la utunzaji wa mazingira kwa jamii ya Mkoa wa Rukwa lilisahaulika sana,Ukataji miti kiholela,Uchomaji Mkaa kwa kasi,Ufanyaji wa shughuli za kilimo zinazohusisha ukataji miti kwa wingi bila kurejesha miti iliyokatwa, Kulima na kufanya shughuli nyingine kwenye milima na Kuchungia mifugo mingi bila uthibiti wa idadi ya mifugo kwenye maeneno muhimu hasa vyanzo vya maji lilikuwa ni suala la kawaida na baadhi ya wananchi hawakujali athari za hayo yote kwa wakati ujao.


 IMEELEZWA kuwa kupitia biashara ya hewa ya ukaa wakazi wake vijiji nane katika  katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi wamepokea zaidi ya Sh bilioni 6.5/- kati ya Julai na Disemba 2022.




Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Makamu was Rais - Mazingira,Dk Switbert Mkama alibainisha yao jana alipokuwa akifungua warsha ya siku mbili iliyofanyika mjini Sumbawanga iliyoratibiwa na Mradi Endelevu wa Mazingira na Uhifahi wa Baioanuai Tanzania -Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira  

Alisema ili kuwajengea uelewa wa urejeshwaji wa mifumo ya Ikolojia na hifadhi ya bionuai kwa madiwani ambao ni wajumbe was kamati za za kudumu za Mazingira kutoka  halmashauri za Sumbawanga (Rukwa) ,Mpimbwe na Tanganyika (Katavi).

 " Nimejulishwa kwamba mwezi Julai
2022,  wakazi wa vijiji nane katika Halmashauri ya Tanganyika wamepokea kutoka kwa kampuni ya Karboni  
shilingi 2,300,000,000 na mwezi Disemba 2022,walipokea shilingi 
4,276,000,000 " alieleza 

Akifafanua alisema kuwa  kati ya fedha hizo asilimia kumi (10) inabaki halmashauri na 
asilimia tisini (90) zinapelekwa kwenye vijiji husika kwa ajili ya shughuli 
mbalimbali za maendeleo.

" Ni dhahiri kwamba wananchi wa vijiji hivyo wameona 
umuhimu wa kuhifadhi misitu na kwavyovyote vile hawawezi kuruhusu mtu 
yeyote kuharibu misitu hiyo" alisisitiza 

Aliwataka madiwani 
kutoka halmashauri za Mpimbwe (Katavi) na Sumbawanga (Rukwa) kutumia fursa ya Mradi   Endelevu wa Mazingira na Uhifahi wa Baioanuai Tanzania 
kuvijumuisha vijiji vinavyotekeleza mradi katika biashara ya hewa ukaa ili nao 
wanufaike. 

Alisema kwa  kufanya hivyo, itasaidia katika kutekeleza kwa ufanisi shughuli 
za mradi lakini pia kusaidia kufikia azma ya Serikali ya kurejesha hekta milioni 
5.2 iliyoahidi kuzirejesha chini ya Mkakati wa Afrika (AFR100) wa kurejesha 
hekta milioni 100 za misitu na ardhi iliyoharibika..

"Aidha niwakumbushe kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita 
inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Samia Suluhu Hassan haitavumilia kuona ubadhilifu wa aina yoyote kwenye Halmashauri zenu katika utekelezajiwa mradi huu" alitahadharisha.

Nae Mratibu wa Mradi wa 
Urejeshaji Endelevu wa Mazingira na Uhifahi wa Baioanuai Tanzania kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Dk Damas Mapunda alisema mradi huo wenye thamani ya Dola za Marekani 11,205,872 unatekelezwa kwa miaka mitano (2021 – 2025),

Akifafanua alisema , mradi huo unaofadhiliwa na Mfuko wa Mazingira wa Dunia (Global 
Environmental Facility-GEF) na unasimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP).


Aidha Katika Mkoa wa Rukwa maeneo ya vilima vya Lyamba Lya Mfipa ni baadhi ya maeneo ambayo yaliharibwa kimazingira kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu kama zilivotajwa hapo awali hivyo serikali imewekeza nguvu kubwa Katika maeneo hayo,kupitia mradi wa Urejeshaji endelevu wa mazingira na uhifadhi wa banuai kwa kuhakikisha Elimu kwanza inawafikiwa wanajamii kujua na kuelewa madhara ya uharibifu wa mazingira,Kupanda miti,kuthibiti ufugaji holela na utunzji wa vyanzo vya maji.


Aidha Mradi unalenga kuangalia mahitaji ya wanajamii kama vile visisma hivyo utaweza kuwa na program za ujenzi wa visimakwa ajili ya kunyweshea mifugo kwenye maeneo yao ili kulinda vyanzo vya maji, kutoa elimu ya kujenga majiko mbadala ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa,Kuboresha mifumo ya maji safi ili kuwapusha wananchi kwenda kabisa kwenye vyanzo vya maji hii itasaidia kulinda mazingira.


Comments

Popular posts from this blog

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MAENDELEO YA CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA