PLAN INTERNATIONAL YACHANGIA VIFAA VYA ELIMU RUKWA
Shirika la Plan International Tanzania limekabidhi msaada wa vitabu, vyoo shirikishi na miundombinu ya maji kwa shule za sekondari na msingi kwenye Halmashauri za Wilaya Nkasi, Kalambo na Sumbawanga vyenye thamani ya shilingi Milioni 786 . Halfa ya makabidhiano ya msaada huo imefanyika katika shule ya msingi Milundikwa wilaya ya Nkasi jana (Januari 19,2023) ambapo Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Sebastian Waryuba alipokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga. Waryuba akizungumza kwenye hafla hiyo alitoa pongezi kwa shirika hilo kwa kuchangia vyoo shirikishi 17 na miundombinu ya maji katika shule za msingi 7 na sekondari 9 katika Wilaya za Nkasi, Sumbawanga Vijijini na Kalambo vyenye jumla ya thamani ya shilingi za kitanzania 716, 607, 527. Plan International imetoa pia vitabu vya kiada 10, 128 kwa shule za msingi 29 za wilaya ya Nkasi vyenye thamani ya shilingi za kitanzania 70, 210, ...