Posts

Showing posts from June, 2022

VIWANJA VYA MICHEZO VIBORESHWE KALAMBO

Image
  Halmshauri ya Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa imetenga ekari 16.9 na fedha kiasi cha shilingi Mil 7 kwa ajili ya kujenga Uwanja wa Mpira wa Miguu katika Mji wa Matai ikiwa ni juhudi za kuweka mazingira bora ya kuimarisha michezo wilayani Kalambo na kutoa fursa ya kuibua vipaji vya soka. Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Shafi Mpenda amesema wilaya ya Kalambo inalengo la kuwa na timu ya soka ya Halmashauri itakayoshiriki ligi kubwa nchini halmashauri yake imetenga ekari 16.9 na fedha shilingi Mil 7 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa uwanja wenye viwango vinavyotakiwa kwa ajili ya mchezo wa soka na michezo mingine. Baadhi ya wadau wa michezo wilayani Kalambo wameomba kujengwa uwanja wenye vigezo vinavyotakiwa vya michezo kwani viwanja vilivyopo havikidhi viwango. Wilaya ya kalambo imeanza kuendesha mashindano ya ligi daraja la nne inayozishirikisha timu 16 kutoka vijiji 111.

Sensa kwa Maendeleo Jiandae Kuhesabiwa

Image
  Shiriki katika Kampeni ya Uhamasishaji ya Sensa ya Watu na Makazi 2022 Tanzania 🇹🇿📍 kwa kubonyeza link hapo chini na kuweka *picha yako* 🙂 kama ishara ya kuunga mkono Sensa ya Watu na Makazi. Baada ya hapo download na share na wengine bila kusahau Hashtag ya #SENSATZ2022 #NIPOTAYARIKUHESABIWA 👇🏽 twb.nz/sensa2022tanzania

TANZANIA KUUNGANA NA NCHI NYINGINE TATU KULINDA ZIWA TANGANYIKA..WASAINI MKATABA

Image
T anzania na nchi zingine tatu zimeweka mkataba wa ushirikiano wa kikanda wa u shirikiano wa ulinzi wa rasilima za uvuvi Katika nchi zinazomiliki ziwa Tanganyika Mkataba huo umezinduliwa na Mhe.Mashimmba Ma s h auri Ndaki Waziri wa Mifugo na Uvuvi katika Kijiji ch Kabwe wilayani Nkasi Mkoani Rukwa na kuwataka Wananchi na wavuvi kwa ujumla kuzingatia malengo ya mkataba huo . Mkataba huo unaohusisha nchi ya Zambia,Burundi, Drc.Kongo na Tanzania unalenga kulilinda ziwa Tanganyika kwa kuhakikisha zana za Uvuvi haramu zinadhibitiwa kama vile Nyavu za kuvulia Samaki na dagaa zinakuwa na vipimo sahihi , Lakini pia kuhakikisha Katika Kila mwaka ziwa linafungwa kwa muda was miezi mitatu ili kuwezesha Samaki kuzaliana.Hayo Ni baadhi tu ya malengo ya mkataba huo. Waziri Mashimba Ndaki amewataka wavuvi kuwa tayari kupokea mabadiriko hayo Katika matumizi ya ziwa Tanganyika ili Kuulinda mazao yanayopatikana Katika ziwa ...

Sensa ya watu na Makazi

Image
 

RC HOMERA ASISITIZA UBUNIFU KWA WAANDISHI WA HABARI

Image
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera akifungua mkutano uliondaliwa na Mfuko wa mawasilino kwa wote ( USCAF) na kuwakutanisha wakurugenzi wa Televisheni za Mtandano na Redio Kutoka katika Mkoa wa Rukwa, Katavi,Njome, Songea na Mbeya ili kujadili kwa pamoja namna ya kuendelea kuboresha huduma za mawasiliano kwa wote ambapo amewataka waandishi wa habari kuhakikisha wanaitendea jamii kwa kuipatia habari zenye ubora na weledi na zinazoendana na kasi ya maendeleo ya teknolojia, Aidha RC Homera amewataka waandishi kuwa wabunifu katika kuandika habari zao ili ziwe na mvuto kwa wasomaji,watazamji na wasikilizaji.

Karibu Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote

Image
  Karibu Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Wapendwa watanzania wenzangu, Ili kufanikisha dira yetu ya: “Kufanikisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano Tanzania kikamilifu na kwa usawa”, Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) unalenga kuimarisha uwezo wa kushirikiana na watoa huduma za mawasiliano nchini ili kuhakikisha ufikiaji wa huduma za mawasiliano katika maeneo yote yenye mawasiliano hafifu pamoja na yale yasiyo na huduma hiyo kabisa. Katika kutekeleza majukumu yake,  Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)   umejielekeza katika kubaini maeneo ya miradi ya mawasiliano ambayo yanaweza kupata ruzuku Serikalini kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, lengo ni kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa na huduma za mawasiliano ambayo kwa kiasi kikubwa yanachangia katika uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Serikali kwa ujumla. Tangu kuanza kazi kwa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) mwaka 2009, kumekuwa na  mafanikio mengi katika sekta ya mawasiliano, ...

TATHMINI YA UTOAJI WA CHANJO YA UVIKO 19 NYANDA ZA JUU KUSINI

  WATAALAM WA AFYA WATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE KUPATA CHANJO YA COVID 19 Na Peter Helatano-Sumbawanga - Rukwa Waatalaamu wa fya katika nyanda za juu kusini wametakiwa kujitokeza na kuwa mstari wa mbele katika kupata chanjo ya uviko 19 ili kuongeza hamasa kwa wananchi kupata chanjo ya corona kutokana na takwimu za zoezi   hilo   kwenye mikoa hiyo kuwa chini ukilingasha na mikoa mingine nchini.   Hayo yamebainishwa na kaimu katibu tawala mkoani Rukwa david kilonzo wakati wa ufunguzi wa kikao cha tathimini ya   zoezi   la utoaji chanjo ya uviko 19   katika mikoa    ya rukwa , katavi na songwe   kikao kilichofanyika mjini sumbawanga. Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi hilo kwenye mikoa ya nyanda za juu kusini mkurugenzi wa shirika la walter reed) Sally Chalamila   akaelezea mafanikio ya zoezi hilo huku mkurugenzi msaidizi elimu ya afya kwa umma kutoka wizara ya afya   dkt. Amalberga Kasangala akisisiza umhimu ...

WATOTO 124,498 KUSAJILIWA KUPATA CHETI CHA KUZALIWA RUKWA

Image
  Na Peter Helatano Mkoa wa Rukwa umefanikiwa kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto 124,498 chini ya mpango wa Usajili wa watoto walio na umri chini ya miaka mitano unaoratibiwa na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) ulioanza Novemba mwaka 2021 . Mafanikio hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti   wakati akifungua kikao cha tathmini kuhusu utekelezaji wa mpango huo kilichofanyika mjini Sumbawanga. Kwa upande wake Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Charles Salyeem alisema Mpango huo umeleta maboresho makubwa katika mfumo wa usajili wa vizazi na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto kwani sasa huduma hiyo inapatikana katika Ofisi za Watendaji Kata na Vituo vya Tiba kote mkoani   Rukwa. . Zoezi hili la usajili wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano linaendelea nchini na hakuna malipo yoyote hivyo ni wazi wanajamii kujitokeza na kuwapeleka watoto kuwasajili.  ...