VIWANJA VYA MICHEZO VIBORESHWE KALAMBO
Halmshauri ya Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa imetenga ekari 16.9 na fedha kiasi cha shilingi Mil 7 kwa ajili ya kujenga Uwanja wa Mpira wa Miguu katika Mji wa Matai ikiwa ni juhudi za kuweka mazingira bora ya kuimarisha michezo wilayani Kalambo na kutoa fursa ya kuibua vipaji vya soka.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Shafi Mpenda amesema wilaya ya Kalambo inalengo la kuwa na timu ya soka ya Halmashauri itakayoshiriki ligi kubwa nchini halmashauri yake imetenga ekari 16.9 na fedha shilingi Mil 7 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa uwanja wenye viwango vinavyotakiwa kwa ajili ya mchezo wa soka na michezo mingine.
Baadhi ya wadau wa michezo wilayani Kalambo wameomba kujengwa uwanja wenye vigezo vinavyotakiwa vya michezo kwani viwanja vilivyopo havikidhi viwango.
Wilaya ya kalambo imeanza kuendesha mashindano ya ligi daraja la nne inayozishirikisha timu 16 kutoka vijiji 111.
Comments
Post a Comment