TANZANIA KUUNGANA NA NCHI NYINGINE TATU KULINDA ZIWA TANGANYIKA..WASAINI MKATABA


T
anzania na nchi zingine tatu zimeweka mkataba wa ushirikiano wa kikanda wa ushirikiano wa ulinzi wa rasilima za uvuvi Katika nchi zinazomiliki ziwa Tanganyika

Mkataba huo umezinduliwa na Mhe.Mashimmba Mashauri Ndaki Waziri wa Mifugo na Uvuvi katika Kijiji ch Kabwe wilayani Nkasi Mkoani Rukwa na kuwataka Wananchi na wavuvi kwa ujumla kuzingatia malengo ya mkataba huo.

Mkataba huo unaohusisha nchi ya Zambia,Burundi,Drc.Kongo na Tanzania unalenga kulilinda ziwa Tanganyika kwa kuhakikisha zana za Uvuvi haramu zinadhibitiwa kama vile Nyavu za kuvulia Samaki na dagaa zinakuwa na vipimo sahihi, Lakini pia kuhakikisha Katika Kila mwaka ziwa linafungwa kwa muda was miezi mitatu ili kuwezesha Samaki kuzaliana.Hayo Ni baadhi tu ya malengo ya mkataba huo.

Waziri Mashimba Ndaki amewataka wavuvi kuwa tayari kupokea mabadiriko hayo Katika matumizi ya ziwa Tanganyika ili Kuulinda mazao yanayopatikana Katika ziwa Hilo kwani kwa Sasa uzalishaji Katika ziwa Tanganyika unepungua kwa kiasi kikubwa Sana kutokana na ziwa kuvuliwa bila kupumzishwa kwa mda mrefu,Uvuvi haramu pamoja nabuhalibifu wa mazingira pembezoni mwa ziwa sehemu ambazo Ni mazalia ya Samaki.

Mkataba huo Katika nchi nyingine ulishazinduliwa hivyo ilikuwa inasubiliwa Tanzania kuuzindua ili kuwa na adhma ya pamoja na muda Katika kulifunga ziwa Tanganyika kwa mda wa miezi mitatu.

Mkataba huo kama utatekelezwa ipasavyo kwa nchi zote utasaidia ongezeko la Samaki na viumbe wengine wa majini Hali itakayosaidia kuinua kipato kwa Wananchi na kusaidia upatikanaji wa Samaki wakubwa tofauti na Hali ilivyo kwa Sasa.

Mhe.Mashimba amewataka Wananchi kujishughulisha na kazi zingine za kuingiza kipato ili ziwa na shuguli za majini zitakapositishwa kwa mda wasiweze kuhangaika.

Comments

Popular posts from this blog

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MAENDELEO YA CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA