WATOTO 124,498 KUSAJILIWA KUPATA CHETI CHA KUZALIWA RUKWA
Na Peter Helatano
Mkoa wa Rukwa umefanikiwa kusajili na
kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto 124,498 chini ya mpango wa Usajili wa
watoto walio na umri chini ya miaka mitano unaoratibiwa na Wakala wa Usajili
Ufilisi na Udhamini (RITA) ulioanza Novemba mwaka 2021 .
Mafanikio
hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti wakati akifungua kikao cha tathmini kuhusu
utekelezaji wa mpango huo kilichofanyika mjini Sumbawanga.
Kwa
upande wake Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini
(RITA) Charles Salyeem alisema Mpango huo umeleta maboresho makubwa katika
mfumo wa usajili wa vizazi na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto kwani sasa
huduma hiyo inapatikana katika Ofisi za Watendaji Kata na Vituo vya Tiba kote
mkoani Rukwa.
.
Zoezi hili la usajili wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto
chini ya umri wa miaka mitano linaendelea nchini na hakuna malipo yoyote hivyo
ni wazi wanajamii kujitokeza na kuwapeleka watoto kuwasajili.
MWISHO.
Comments
Post a Comment