Posts

Mtumishi Halmashauri Ya Kalambo Mbaroni Kwa Kukutwa Na Mashine Bandia Ya Ukusanyaji Mapato.

Image
   Na Baraka Lusajo - Kalambo  Jeshi la polisi Mkoani Rukwa linamshikilia Timoth Ngambeki ambae ni mtumishi wa Halmashauri ya Kalambo kwa tuhuma za kutumia mashine bandia na kutoa risiti feki kwa wananchi na kuisababishia serikali hasara ya shilling million thelathini na tisa na laki tano. Mapema akiongea ofisini kwake mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Kalambo Shafi Mpenda alisema mtumishi huyo aligundulika kufanya kitendo hicho baada ya kushindwa kuwasilisha fedha Benk na kwamba baada ya ufuatiliaji zaidi kwenye mageti ya ukusanyaji mapato aligundua uwepo wa udanganyifu kwenye utoaji wa risiti. ‘’baada ya kugundua uwepo wa udanganyifu kwenye swala la ukusanyaji mapato nilianzisha utaratibu wa kuweka madaftari ya kusaini kwenye mageti yote yanayo unganisha halmanshauri za jirani na kuweka watu ambao walikuwa wakifanya kazi ya kupiga picha risiti za ushuru kisha kunitumia na wakati mwingine nilikuwa nikiamka usiku na kufuatilia mwenendo wa ukusanyaji mapato kwenye mag...

Mkurugenzi UTPC awataka Waandishi kuandika Habari za Usawa wa kijinsia ili kuleta mabadiliko Chanya katika jamii.

Image
  Na.Neema Mtuka Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania(UTPC) Bw.Kenneth Simbaya amewataka Waandishi wa Habari kuendelea kuandika Habari za Usawa wa kijinsia ili kuleta mabadiliko Chanya kwa jamii. Simbaya ameyasema hayo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari za Usawa wa kijinsia yaliyo wakutanisha Waandishi wa Tanzania Bara na visiwani. Ameongeza kuwa Waandishi wanapaswa kuibua Habari za ukatili wa kijinsia ambazo zitasaidia jamii kubadili mitazamo hasi na kuachana na Mila potofu zilizopitwa na wakati ambazo Bado Zina mkandamiza mwanamke na kupotea maana ya Usawa wa kijinsia  Aidha amesema Waandishi wa Habari washirikiane kwa pamoja katika kuibua mambo mbalimbali yahusuyo jamii na kufanya kazi kwa pamoja na kuhakikisha wanazingatia maadili ya uandishi wa Habari kanuni na taratibu zilizopo. Mafunzo ya Usawa wa kijinsia yanafanyika mjini Morogoro ambapo pamoja na mambo mengine Waandishi wanatazamia kuleta mabadiliko makubwa k...

Msimamo wa Nchi ni kulinda Uhuru wa Vyombo vya Habari

Image
 Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhe.Nape Nnauye amesema msimamo wa thabiti wa Nchi ya Tanzania ni kulinda Uhuru wa Vyombo vya Habari,na ndio mana Serikali iliamua kufanya marekebisho ya Sheria ya huduma ya Habari Sura ya 229,ili ikidhi Uhuru wa vyombo vya Habari. Mhe .Nape amesema hayo Leo Julai 31,2023 jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua kozi fupi ya 15 ya Wahariri wa vyombo vya Habari inayotolewa na chuo Cha Taifa Cha Ulinzi. "Wanahabari niwahakikishieni msimamo thabiti wa Nchi yetu ni kulinda Uhuru wa vyombo vya Habari.Mh.Rais mara nyingi amekuwa akiagiza kufanya kazi bila kuingilia Uhuru wa vyombo vya Habari",amesema Mh.Nape. Aidha amewataka Wahariri hao mara watakapomaliza  kozi hiyo na kurudi katika vituo vyao vya  kazi,wafanye kazi kwa kuangalia maslahi ya nchi,vilevile amewataka kuendelea kulifanya Taifa kuwa kitu kimoja na Kukuza Umoja wa Taifa. Kwa upande wake kansela wa chuo Cha Taifa Cha Ulinzi,Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee amesema kuwa ...

Watumishi Wa Umma Wilayani Kalambo Waungana Kuadhimisha Kumbukizi Ya Mashujaa Kwa Kufanya Usafi.

Image
  Watumishi wa Umma wilayani Kalambo mkoani Rukwa wameungana na watu wengine katika kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya mashujaa kwa kufanya usafi kwenye majengo ya hospitali ya wilaya  hiyo ili kuendeleza kampeni ya usafi wilayani humo. Zoezi hilo liliongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Lazaro Komba alisisitiza kuwa zoezi hilo ni endelevu kwa kila siku ya mwisho wa mwezi ili kukabiliana na magonjwa ya milipuko ikiwemo kipindupindu na magonjwa ya kuhara. Komba alisisitiza wananchi kujenga mazoea kufanya usafi wa mazingira kuzunguma maeneo yao husika kwa lengo la kuifanya wilaya kuwa safi muda na wakati wote. ‘’Kimsingi leo tumekutana kufanya usafi hapa kwenye majengo ya Hospitali ya wilaya Kalambo kama  sehemu ya kuadhimisha kumbukizi ya siku ya mashujaa na maadhimisho haya kwa ngazi ya kitaifa yanafainyika mkoani Dodoma’’ alisema komba. Mapema akiongea na Watumishi wa umma wakati wa shughuli za usafi kwenye maeneo hayo ,Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Shafi ...

WATOTO WATATU FAMILIA MOJA WAFA MAJI WAKIVUA SAMAKI KATAVI

Image
  Na.Mary Clemence,Katavi Watoto watatu wa familia Lucia Kazima(10),Kabisi Lazima(8),na Makala Lazima(6) wakati wa kitongoji Cha Kayenze B Wilayani Mpanda wamekufa Maji wakati wakivua samaki katika mto Kamilala. Watoto hao walikuwa wanafunzi wa shule ya msingi Kamilala ambapo Lucia alikuwa akisoma darasa la 5,Kabisi darasa la nne na Makala darasa la kwanza. Kamanda wa polisi Mkoa wa Katavi,Kaster Ngonyani akizungumza na Waandishi wa Habari Leo jumatano Julai 19,2023 amesema tukio Hilo limetokea Julai 13,2023 saa 7:45 mchana. "Eneo la mto huo linatumika pia kwa shughuli za uvuvi samaki,watoto hao walikwenda kuvua samaki,haikufahamika kama walikuwa wanaogelea au ilikuwaje,"amesema. "Kwa sababu hii miili Yao ilikutwa ikielea na wasamalia wema walitoa taarifa polisi Kisha iliopolewa na kufanyiwa Uchunguzi Kisha ndugu wakakabidhiwa kwa ajili ya taratibu za maziko,"amesema Kaster. Kamanda Ngonyani ametoa Rai kwa wazazi na walezi kuwa na uangalizi wa karibu pindi watoto wa...

HUDUMA YA KITI MWENDO YAANZISHWA KITUO CHA DALADALA MUHIMBILI.

Image
 Hospital ya Muhimbili imeanzisha huduma ya kubeba wagonjwa wasioweza kutembea kutoka kwenye kituo Cha daladala kilichopo nje ya geti la kuingilia hadi katika maeneo ya kutolea huduma kwa kutumia Viti mwendo(wheel chairs). Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za uuguzi na ukunga wa MNH,Bi.Redempta  Matindi amesema kuwa huduma hiyo ni muhimu kwa kuwa wapo wagonjwa wasiojiweza kabisa kutembea wenyewe. "Sisi kama watoa huduma tumeona ni vema kuanzisha huduma hii kuwasaidia mwendo wagonjwa ili wafike kwenye maeneo ya kutolea huduma wakishafika huko wanakutana na watoa huduma wa maeneo husika"amesema Bi Redempta. Amesema huduma hizo zinatolewa na waliokuwa waraibu wa dawa za kulevya ambao wanaendelea na tiba ya Methadone ili kuwasaidia kurejea katika maisha ya kawaida.

KASULU DC YAENDELEZA UUNDAJI WA KLABU ZA LISHE

Image
 Na Mwandishi wetu. Katika kuendelea kuboresha Afya ya Jamii Halmashauri ya Wilaya Kasulu kupitia kwa wataalamu wa lishe inaendelea kuunda Klabu za lishe mashuleni ambazo zitasaidia kutoa Elimu ya masuala ya lishe,kwa kuanzisha bustani za mbogamboga na matunda. Akitoa ripoti hiyo Leo katika kikao Cha lishe kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo Afisa Lishe Kingolo Sayi amesema Hali ya uwepo wa Klabu za lishe ni asilimia 43 kwa shule za msingi na asilimia 75 kwa shule za sekondari. Sayi ameongeza kuwa katika kuimarisha uungwaji wa Klabu hizo mashuleni,vijiji 24 katika kata 15 vimehamasishwa juu ya umuhimu wa Klabu shuleni. Itakumbukwa kuwa uwepo wa Klabu za lishe shuleni zinasaidia kutoa Elimu kwa wanafunzi a jamii juu ya umuhimu wa lishe Bora na ushiriki wake.