Mkurugenzi UTPC awataka Waandishi kuandika Habari za Usawa wa kijinsia ili kuleta mabadiliko Chanya katika jamii.
Na.Neema Mtuka
Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania(UTPC) Bw.Kenneth Simbaya amewataka Waandishi wa Habari kuendelea kuandika Habari za Usawa wa kijinsia ili kuleta mabadiliko Chanya kwa jamii.
Simbaya ameyasema hayo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari za Usawa wa kijinsia yaliyo wakutanisha Waandishi wa Tanzania Bara na visiwani.
Ameongeza kuwa Waandishi wanapaswa kuibua Habari za ukatili wa kijinsia ambazo zitasaidia jamii kubadili mitazamo hasi na kuachana na Mila potofu zilizopitwa na wakati ambazo Bado Zina mkandamiza mwanamke na kupotea maana ya Usawa wa kijinsia
Aidha amesema Waandishi wa Habari washirikiane kwa pamoja katika kuibua mambo mbalimbali yahusuyo jamii na kufanya kazi kwa pamoja na kuhakikisha wanazingatia maadili ya uandishi wa Habari kanuni na taratibu zilizopo.
Mafunzo ya Usawa wa kijinsia yanafanyika mjini Morogoro ambapo pamoja na mambo mengine Waandishi wanatazamia kuleta mabadiliko makubwa katika jamii.
Comments
Post a Comment