Posts

Ahukumiwa Mwaka Mmoja Na Nusu Kwa Kosa La Wizi

Image
  Na baraka  Lusajo  - Rukwa Mahakama ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa imemuhukumu kwenda jela mwaka mmoja na nusu Frank Geoffrey Sikazwe (28) mkazi wa kijiji cha Kasanga wilayani humo kwa kosa la wizi. Mtuhumiwa alishitakiwa kwa makosa mawili baada ya   kuvunja nyumba ya Lauriano Simbeye huko Kasanga usiku wa tarehe 05 Februari 2020, akiwa na kusudio la kuiba kinyume na kifungu 294(1)(a) and (2) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya mwaka 2019, pia kosa la wizi kinyume na kifungu 258(1)(2)(a) na 265 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya mwaka 2019. Mtuhumiwa alikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi Matai na kuandaliwa hati ya mashitaka hatimaye kufikishwa mahakamani. Baada ya kusomewa mashitaka alikana kutenda kosa hilo suala lililopelekea upande wa mashitaka kuwa na jukumu la kuthibitisha pasi na shaka tuhuma zinazomkabili mshitakiwa.   Upande wa mashitaka ukiongozwa na mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi Mrisho Kimbeho...

Bongo Movie na Bongo Fleva wakutanishwa kwenye Michezo kuamua mbabe.

Image
 Na Baraka Lusajo. Rukwa Katika kuendeleza na kukuza amani, upendo, mshikamano na kudumisha umoja kwa wasanii wanaoigiza maarufu kama “Bongo Movie” pamoja na wasanii waimbaji maarufu kama “Bongo Fleva”, Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa Kiheka Charles amezikutanisha timu za makundi hayo mawili katika mechi ya mpira wa miguu iliyopigwa katika viwanja vya shule ya sekondari Mazwi mjini Sumbawanga. “Michezo ni Afya, Sanaa ina kazi ya kuelimisha na kuburudisha, sanaa huifanya jamii kuwa kitu kimoja, na michezo pia huifanya jamii kuwa kitu kimoja na tunashirikiana katika mambo mbalimbali hasa katika kutangaza kampeni zetu mbalimbali za kimaendeleo, kutangaza fursa zinazopatikana ndani ya manispaa yetu ya Sumbawanga na tukifanya vizuri, unajua ile sumbawanga iliyokuwa inasifika zamani ile sifa itapotea, nadhani wenye mnaona watu wakija kutoka mbali wanaona tofauti na walivyokuwa wanafikiria,” Alisema  Kiheka. Kwa upande wao washiriki wa mchezo huo waliishuku...

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

Image
Na  Baraka Lusajo - Rukwa. Vyama vya Ushirika wilayani Kalambo mkoani Rukwa vimetakiwa kuwekeza nguvu zao katika upatikanaji wa zana bora za kilimo ili kuweza kuongeza uzalishaji na ubora wa mazao mbalimbali mkoani Rukwa hasa katika kipindi hiki wanachojiandaa kuanza msimu mpya wa kilimo unaotarajiwa kuanza mwezi Oktoba mwaka huu.   Akiongea wakati wa Ufunguzi wa uzinduzi wa Mkakati wa matumizi bora ya zana za kilimo, Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Rukwa, Ocran Chengula alisema kuwa, asilimia 80 ya uchumi wa Mkoa wa Rukwa unategemea kilimo lakini ni asilimia 3 tu ya wakulima wanatumia matrekta hali inayopekelea eneo kubwa la ardhi inayofaa kulimwa katika mkoa huo kutolimwa na pia kutopata mazao bora yenye kuhimili ushindani katika soko la dunia. “Katika mkoa wetu kuna hekta 1,660,000 ambazo zinafaa kwa kilimo, lakini kati ya hizo kwa kiasi kikubwa sana tunazoloma ni hekta laki tano na kidogo, ambazo ni sawa na asilimia 32 kuna kipi...

Maelfu Ya Waumini Wajitokeza Kuombea Uchaguzi''kalambo.''

Image
Na Baraka Lusajo. Rukwa Waamini pamoja   na wachungaji kutoka   madhehebu mbalimbali   ya   dini kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama wilayani   Kalambo mkoani Rukwa, wameungana kuendesha   kongamano la   kumuomba mwenyezi Mungu ili uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu, uwe wa haki   ili kuilinda amani na utulivu uliopo kwa lengo la   kuivusha nchi ikiwa salama bila   kumwaga damu. Makamu askofu wa kanisa la FPCT jimbo la   Rukwa na katavi Andrea   Mwakalinga   amesema   watumishi   wa   Mungu   tunahitaji kamapeni safi bila   ugomvi   na kwamba kufanya fujo   ni   kukosa hekima   ya   kimungu. Amesema   kwa kuwa   wagombea   wote wanatoka   katika makanisa na misikiti   yetu, Mashehe na Wachungaji tuta hakikisha tuna hubiri amani na utulivu kwenye mihadhara   yetu. ‘’sisi t...

Msimamizi wa uchaguzi Jacob Mtalitinya akimkabidhi fomu ya kugombea Ubunge, ndg Julius Mizengo mgombea kupitia chama wa wananchi CUF.

Image
 

CUF WAJITOSA KUCHUKUA FOMU YA UBUNGE SUMBAWANGA MJINI

Image
Baada ya kusuasua kwa zoezi la kuchukua kwa siku mbili, hatimaye Mgombea wa CUF, Julius Mizengo awa wa kwanza kuchukua fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Sumbawanga Mjini.

Wandishi Wa Habari Mkoani Rukwa Wachagua Viongozi Wapya.

Image
KATIKA  PICHA NI WANACHAMA WA RUKWA PRESS WAKIWA KWENYE  CHUMBA CHA UCHAGUZI Na  Baraka Lusajo . Rukwa CHAMA cha Waandishi wa Habari mkoani Rukwa (RKPC) kimepata viongozi wapya watakao kiongoza Chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.  Uchaguzi huo umefanyika Jana kwenye ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga ambapo Waandishi wa Habari walitumia demokrasia yao kupitia uchaguzi ambao uliangaliwa na mjumbe wa bodi UTPC Andrew Kuchonjoma na Mwakilishi wa katibu tawala wa mkoa Emmanuel Kakwezi. KATIKA PICHA NI WANACHAMA WAKIWA KWENYE CHUMBA CHA UCHAGUZI  Mwenyekiti wa Baraza la uchaguzi Cresensia Daimon alimtangaza Swima Ernest kushinda nafasi ya Mwenyekiti kwa kupata kura 17 za ndiyo huku kura 9 za hapana, Makamo mwenyekiti ni Israel Mwaisaka aliyepata kura 13 dhidi ya mpinzani wake Emmanuel Mayunga Aliyepata kura 11,nafasi ya katibu mkuu ilinyakuliwa na Sammy Kisika aliyepata kura 25 za ndiyo ambapo alipata Kura 1 ya hapana kwa kuwa hakua na mpin...