Bongo Movie na Bongo Fleva wakutanishwa kwenye Michezo kuamua mbabe.

 Na Baraka Lusajo. Rukwa

Katika kuendeleza na kukuza amani, upendo, mshikamano na kudumisha umoja kwa wasanii wanaoigiza maarufu kama “Bongo Movie” pamoja na wasanii waimbaji maarufu kama “Bongo Fleva”, Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa Kiheka Charles amezikutanisha timu za makundi hayo mawili katika mechi ya mpira wa miguu iliyopigwa katika viwanja vya shule ya sekondari Mazwi mjini Sumbawanga.

“Michezo ni Afya, Sanaa ina kazi ya kuelimisha na kuburudisha, sanaa huifanya jamii kuwa kitu kimoja, na michezo pia huifanya jamii kuwa kitu kimoja na tunashirikiana katika mambo mbalimbali hasa katika kutangaza kampeni zetu mbalimbali za kimaendeleo, kutangaza fursa zinazopatikana ndani ya manispaa yetu ya Sumbawanga na tukifanya vizuri, unajua ile sumbawanga iliyokuwa inasifika zamani ile sifa itapotea, nadhani wenye mnaona watu wakija kutoka mbali wanaona tofauti na walivyokuwa wanafikiria,” Alisema  Kiheka.

Kwa upande wao washiriki wa mchezo huo waliishukuru Ofisi ya Mkurugenzi Manispaa ya Sumbawanga kwa uratibu wa mchezo huo uliofanywa na afisa utamaduni wa manispaa hiyo huku wakiendelea kusisitiza wadau wengine wajitokeze katika kukuza michezo kwani michezo huleta furaha katika jamii.  

Pia kapteni wa timu ya Bongo fleva Steven Stanley a.k.a Young Steve alimpongeza Afisa utamaduni huyo kwa juhudi za kuwakutanisha wasanii pamoja,

 

 

Comments

Popular posts from this blog

Watumishi Wa Umma Wilayani Kalambo Waungana Kuadhimisha Kumbukizi Ya Mashujaa Kwa Kufanya Usafi.

Dc Kalambo Ataka Walio Husika Kumuozesha Mwanafunzi Wa Darasa La Saba Kukamatwa

Mkurugenzi UTPC awataka Waandishi kuandika Habari za Usawa wa kijinsia ili kuleta mabadiliko Chanya katika jamii.