Maelfu Ya Waumini Wajitokeza Kuombea Uchaguzi''kalambo.''
Na Baraka Lusajo. Rukwa
Waamini pamoja na wachungaji kutoka madhehebu mbalimbali ya dini kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama wilayani Kalambo mkoani Rukwa, wameungana kuendesha kongamano la kumuomba mwenyezi Mungu ili uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu, uwe wa haki ili kuilinda amani na utulivu uliopo kwa lengo la kuivusha nchi ikiwa salama bila kumwaga damu.
Makamu
askofu wa kanisa la FPCT jimbo la Rukwa
na katavi Andrea Mwakalinga amesema watumishi
wa Mungu tunahitaji kamapeni safi bila ugomvi
na kwamba kufanya fujo ni kukosa hekima
ya kimungu.
Amesema
kwa kuwa wagombea
wote wanatoka katika makanisa na
misikiti yetu, Mashehe na Wachungaji tuta
hakikisha tuna hubiri amani na utulivu kwenye mihadhara yetu.
‘’sisi tuna watu wengi wanao tufuata makanisani na misikitini mwetu, hivyo hatunabudi kuhimiza upendo ili zifanyike kamapeni zisizo na ugonvi kwenye majukwaa ya siasa. Na ijulikane kuwa mtu yeyote atakaye fanya kampeni za fujo kuelekea uchaguzi huu, atakuwa hana nia njema katika ustawi wa nchi yetu.’’ Amesema mwakalinga.
Shehe wa wilaya hiyo Sulemani Amani, alisema kila mtu amefika katika eneo hilo kwa lengo la kufanya maombi na kuwataka washirika wote kuomba katika roho na kweli ili kuhakikisha maombi hayo yanafika kwa mwenyezi mungu kama ilivyo kusudiwa.
Mkuu
wa wilaya ya Kalambo Calorius Misungwi, amesema kila mwananchi anatakiwa kuchagua viongozi bora baada ya kusikiliza sera zao.
‘’Sisi
kazi yetu kama wananchi ni kusikiliza sera na kuchagua
viongozi wenye sifa safi. Hivyo wote
tuhamasike na tujitokeze kwa wingi kuchagua
viongozi bora ambao watakuwa
msaada kwa wilaya na taifa kwa
ujumla.’’ Amesisitiza Misungwi.
Comments
Post a Comment