Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo
Na Baraka Lusajo - Rukwa.
Vyama vya Ushirika
wilayani Kalambo mkoani Rukwa vimetakiwa kuwekeza
nguvu zao katika upatikanaji wa zana bora za kilimo ili kuweza kuongeza
uzalishaji na ubora wa mazao mbalimbali mkoani Rukwa hasa katika kipindi hiki
wanachojiandaa kuanza msimu mpya wa kilimo unaotarajiwa kuanza mwezi Oktoba
mwaka huu.
“Katika mkoa wetu kuna hekta 1,660,000 ambazo
zinafaa kwa kilimo, lakini kati ya hizo kwa kiasi kikubwa sana tunazoloma ni
hekta laki tano na kidogo, ambazo ni sawa na asilimia 32 kuna kipindi tulifika
hadi asilimia 35 lakini ni kiasi kidogo sana, na kitu ambacho kinatukwamisha
katika kuongeza eneo la kilimo ni kutumia zana ambazo sio Rafiki kwa kilimo,
katika mkoa wetu kwa kiasi kikubwa sana (75%) tunatumia zana za kukokotwa na
ng’ombe kwa maana ya maksai,” Alisema.
Wakati akielezea mpango wa serikali kuhakikisha wanavitumia vyama vya ushirika ili kuwawezesha wakulima wadogo wadogo kulima kwa tija, Mrajisi wa Vyama vya Ushirika mkoani Rukwa Benjamin Mangwala alisema kuwa, Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini imeridhia vyama hivyo kuingia mikataba ya mauziano na matumizi ya zana bora za kilimo na makampuni ya usambazaji wa zana hizo ili kuondokana na matumizi ya zana duni huku akifafanua sheria zitakazolinda mikataba hiyo.
“Hiyo sheria ya Ushirika ya mwaka 2013
inaekeleza kwamba maamuzi ya kuweza kununua hayo matreka yatatokana na maamuzi
ya wanachama husika na si vinginevyo kwa maana nyingine ni kwamba pale ambapo
azimio litafanyika wakati mahudhurio ya wanachama yapo chini kwa mujibu wa
sheria, azimio hilo halitakuwa halali na hivyo chama husika kitaathirika kwa
kushindwa kukidhi sifa za hilo azimio, hata kama walikuwa na sifa ya kupata
hicho kifaa, hivyo niwaombe viongozi wa vyama vya ushirika na maafisa ushirika
mshirikiane,” Alieleza.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa kampuni ya
Agricom African Limited alisema kuwa wameamua kufika mkoani Rukwa baada ya
kuona wakulima wengi wanashindwa kulima kwa tija kutofikia malengo kwasababu ya
kukosa zana bora za kilimo ambazo kampuni hiyo inaagiza na kuzisambaza kwa
wakulima.
Miongoni mwa wafaidika wa elimu hiyo ya matumizi bora ya zana za kilimo Mwenyekiti wa Kanyele AMCOS Esther Sikozi alisema kuwa ujio wa vifaa hivyo utawapunguzia kazi kwani ukilimakwa kutumia Wanyama kazi unatumia siku mbili hati tatu kumaliza ekari moja wakati trekta linatumia dakika chache kulima ekari moja.
Mkoa wa Rukwa una vyama vya ushirika 166 huku
88 vikiwa vinajihusisha na kilimo na ni vyama 29 pekee ndivyo vyenye sifa za
kukopesheka na hiyo ni baada ya kuvuka kigezo cha kuwa na idadi kadhaa ya
wanachama ambao wanaweza kuchangia ili kuweza kulipa mkopo wa trekta la
kulimia.
Comments
Post a Comment