Posts

TAKUKURU YAIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA KATIKA KONGAMANO LA 5 LA GLOBE NETWORK NCHINI CHINA

Image
 Being,China -Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU)inashiriki kongamano la 5 la kimataifa la mashirikiano katika mapambano dhidi ya rushwa,linaloendelea jijini Beijing China. Kongamano hili limewakutanisha mamlaka 219 kutoka nchi 121 duniani,likilenga kubafilishana uzoefu na utaalamu katika jukumu la kuzuia na kupambana na rushwa  Kongamano hili la siku Tano limejumuisha warsha ya viongozi wa mamlaka za kuzuia na kupambana na rushwa(high level Forum),ambapo Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU ,Bw.Crispin Francis Chalamila,amewasilisha mada kuhusu "mfumo wa Sheria wa Tanzania katika mapambano dhidi ya rushwa"katika mada yake Bw.Chalamila ameeleza jinsi ambavyo serikali ya Tanzania imekuwa ikijipambanua katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kuimarisha mifumo ya Sheria na ya kitaasisi.Alibainisha uanzishwaji wa divisheni ya mahakama kuu inayoshughulikia masuala ya rushwa na uhujumu uchumi kuwa ni hatua muhimu katika kuhakikisha uwajibikaji na utawala Bora. TAKUKURU

CHONGOLO AIPONGEZA HALMASHAURI YA KALAMBO KUANZISHA TEKNOLOJIA MPYA YA UKAUSHAJI WA DAGAA NA SAMAKI

Image
 Na Neema Mtuka. Mkuu wa mkoa Songwe Mhe.Daniel Chongoro ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa kwa kuanzisha teknolojia mpya ya UKAUSHAJI wa DAGAA na SAMAKI kwa kutumia kaushio la kisasa (Solar tent drier)ambalo litawezesha upatikanaji wa samaki na dagaa wenye ubora na kuwezesha wavuvi kujikwamua na Hali ya kiuchumi. Ameyasema hao baada ya kutembelea Banda la Halmashauri ya Wilaya Kalambo kupitia maonesho ya wakulima nanenane yanayofanyika kikanda jijini Mbeya na kuipongeza Halmashauri ya Wilaya Kalambo kwa kuanzisha teknolojia hiyo ambayo itawezesha kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi baada ya kuvuliwa hususani kipindi Cha masika. Awali akitoa taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo Shafi Mpenda ,Afisa uvuvi Wilayani humo Bw.Abdul Balozi,Amesema sambamba na teknolojia hiyo pia wameleta bidhaa mpya ya unga wa samaki ambayo ni ya kwanza kwa Kanda ya nyanda za juu kusini ambayo itasaidia  kupunguza udumavu na utapiamlo kwa watoto kutokana na unga huo k

BALOZI WA SWEDEN NCHINI ATEMBELEA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI KILIMANJARO

Image
  Mwandishi wetu Jana Agosti 5,2024 Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh.Charlotta Ozaki Macias ametembelea klabu ya waandishi wa Habari Kilimanjaro (MECKI) kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na klabu hiyo pamoja na kufanya mazungumzo na wanachama wa klabu hiyo. Mh.Balozi pia ametaka kujua mchango wa MECKI kwa jamii katika kupaza sauti Ili kuibua Changamoto zilizopo kwenye jamii na namna klabu hiyo ilivyojipanga kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu 2025. Pamoja na mambo mengine Mh.Balozi na wanachama hao wamejadiliana masuala mbalimbali ikiwemo uhuru wa Vyombo vya Habari na namna ya kuandika Habari za uchunguzi. Aidha Mh. Charlotta ameambatana na timu kutoka Muungano wa klabu za waandishi wa Habari Tanzania (UTPC)iliyokuwa ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Kenneth Simbaya.

RAIS WA UTPC AFURAHISHWA NA UBUNIFU WALIOONESHA WAANDISHI WA HABARI

Image
 Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania(UTPC)  Deogratius Nsokolo akiwa ameambatana na Wajumbe wa bodi ya UTPC wametembelea mabanda ya maonesho ya kazi wanazofanya wanachama  wa Umoja huo na kujionea namna ambavyo Waandishi wanafanya kazi za kihabari na kuibua changamoto kwenye jamii. Nsokolo amefurahishwa na namna ambavyo Waandishi wamekuwa wabunifu katika maonesho hayo ambayo yamefanyika katika viwanja vya Ofisi ya UTPC jijini Dodoma. Aidha Nsokolo amesema kupitia maonesho hayo Waandishi wameweza kuonesha shughuli za kiuchumi wanazozifanya na kujikita katika Habari za uchunguzi. Kwa upande wa mwakilishi wa Shirika la Twaweza ambao wamejikita katika kufanya tafiti za Sauti za Waandishi wa Habari Bi.Jane Shussa amesema ili Vyombo vya  habari viweze kupiga hatua na kuweza kujitegemea ni Lazima wao waweze kubadilika na kuandika Habari zenye ukweli. Naye,Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC Kenneth Simbaya amesema maonesho hayo yamekuwa na faida kubwa na kuahidi kuwa mwaka ujao kuy

UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

Image
 Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Deogratius Nsokolo amesema ili kusaidia kupunguza hali ya uhasama dhidi ya Waandishi wa Habari UTPC inaendelea kutumia Klabu za Waandishi wa Habari mikoani kuhamasisha na kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa Uhuru wa  vyombo vya Habari na jukumu la Waandishi wa Habari katika jamii.  Nsokolo ameyasema hayo Leo Novemba 2,2023 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa siku ya Kimataifa ya kukomesha Uhalifu dhidi ya Waandishi wa Habari ulioandaliwa na UTPC na kufanyika kwa njia ya mtandao(Zoom). Amesema maadhimisho hayo kwa mwaka 2023 yanalenga Kuongeza uelewa kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo Waandishi katika kutekeleza majukumu Yao,lakin pia kuonya juu ya kukithiri kwa vitendo vya kikatili na ukandamizaji dhidi ya Waandishi wa Habari. Aidha akiongelea kujenga Mazingira salama kwa Waandishi wa Habari amewashukuru ubalozi wa Uswiss hapa Nchini Tanzania,kwa ufadhili wao katika mradi na Mkuu wa jeshi la polisi Nchini IGP Camilius Wam

WAZIRI MKUU ATIMIZA AHADI YAKE KWA REYO

Image
 Taasisi ya vijana inayojishughulisha na utunzaji wa Mazingira mkoani Rukwa(Rukwa Environmental Youth Organization-REYO)imekabidhiwa Pikipiki ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa mapema mwaka huu alipofanya ziara katika Mkoa wa Rukwa. Amikabidhi Pikipiki hiyo kwa niaba ya Waziri Mkuu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Charles Makongoro Nyerere ameishukuru ofisi ya Waziri Mkuu kwa kutimiza ahadi hiyo kwa Taasisi ya REYO. Ameipongeza Taasisi hiyo kwa kuendelea kutunza Mazingira na kuhamasisha wananchi kutunza Mazingira kwa kutokata miti na kuchoma moto hovyo misitu iliyopo. Akipokea Pikipiki hyo kwa niaba ya Taasisi ya REYO,Be.Issa Rubega amemshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa msaada huo ambao itasaidia kuendelea kampeni Ya utunzaji Mazingira kwa kuwa Pikipiki hiyo itasaidia kufika kwa urahisi na haraka katika maeneo yote.

ZIMAMOTO YATOA MAFUNZO KWA WATUMISHI RUKWA.

Image
 Jeshi la zimamoto Mkoani Rukwa limetoa mafunzo ya uokozi,kujikinga na kukabiliana na majanga ya moto kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa. Mafunzo hayo yaliandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na jeshi la zimamoto Mkoa wa Rukwa yakiwa na lengo la kuwapa watumishi wa umma ujuzi wa kuzuia,kuthibiti na kukabiliana vyema na majanga ya moto. Mafunzo hayo yalitofanyika oktoba 12,2023 yamehusisha utoaji wa Elimu juu ya hatua mbalimbali ya za kukabiliana na majanga ya moto,taratibu za uokoaji,na Matumizi sahihi ya vifaa vya kuzima moto na huduma ya kwanza. Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa,Bi .Sabina Msongela Kaimu Katibu Tawala utawala na usimamizi wa rasilimali watu Mkoa wa Rukwa amewashukuru watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushiriki mafunzo hayo.Amesema kuwa Mafunzo hayo yataongeza kujiamini kwa watumishi wa umma katika kuzuia na kuthibiti majanga ya moto. Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Rukwa limeipongeza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa kuan