ZIMAMOTO YATOA MAFUNZO KWA WATUMISHI RUKWA.

 Jeshi la zimamoto Mkoani Rukwa limetoa mafunzo ya uokozi,kujikinga na kukabiliana na majanga ya moto kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa.

Mafunzo hayo yaliandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na jeshi la zimamoto Mkoa wa Rukwa yakiwa na lengo la kuwapa watumishi wa umma ujuzi wa kuzuia,kuthibiti na kukabiliana vyema na majanga ya moto.

Mafunzo hayo yalitofanyika oktoba 12,2023 yamehusisha utoaji wa Elimu juu ya hatua mbalimbali ya za kukabiliana na majanga ya moto,taratibu za uokoaji,na Matumizi sahihi ya vifaa vya kuzima moto na huduma ya kwanza.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa,Bi .Sabina Msongela Kaimu Katibu Tawala utawala na usimamizi wa rasilimali watu Mkoa wa Rukwa amewashukuru watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushiriki mafunzo hayo.Amesema kuwa Mafunzo hayo yataongeza kujiamini kwa watumishi wa umma katika kuzuia na kuthibiti majanga ya moto.

Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Rukwa limeipongeza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa kuandaa mafunzo hayo muhimu kwa watumishi katika kuzuia majanga ya moto kwa ofisi za umma.








Comments

Popular posts from this blog

Watumishi Wa Umma Wilayani Kalambo Waungana Kuadhimisha Kumbukizi Ya Mashujaa Kwa Kufanya Usafi.

Dc Kalambo Ataka Walio Husika Kumuozesha Mwanafunzi Wa Darasa La Saba Kukamatwa

Mkurugenzi UTPC awataka Waandishi kuandika Habari za Usawa wa kijinsia ili kuleta mabadiliko Chanya katika jamii.