TAKUKURU YAIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA KATIKA KONGAMANO LA 5 LA GLOBE NETWORK NCHINI CHINA

 Being,China -Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU)inashiriki kongamano la 5 la kimataifa la mashirikiano katika mapambano dhidi ya rushwa,linaloendelea jijini Beijing China.

Kongamano hili limewakutanisha mamlaka 219 kutoka nchi 121 duniani,likilenga kubafilishana uzoefu na utaalamu katika jukumu la kuzuia na kupambana na rushwa 

Kongamano hili la siku Tano limejumuisha warsha ya viongozi wa mamlaka za kuzuia na kupambana na rushwa(high level Forum),ambapo Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU ,Bw.Crispin Francis Chalamila,amewasilisha mada kuhusu "mfumo wa Sheria wa Tanzania katika mapambano dhidi ya rushwa"katika mada yake Bw.Chalamila ameeleza jinsi ambavyo serikali ya Tanzania imekuwa ikijipambanua katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kuimarisha mifumo ya Sheria na ya kitaasisi.Alibainisha uanzishwaji wa divisheni ya mahakama kuu inayoshughulikia masuala ya rushwa na uhujumu uchumi kuwa ni hatua muhimu katika kuhakikisha uwajibikaji na utawala Bora.

TAKUKURU ilipewa nafasi ya pekee kutoa wasilisho,ikiwa ni miongoni mwa nchi 70 zilizoteuliwa kufanya hivyo,ikionesha nafasi ya kipekee ambayo Tanzania inachukua katika mapambano haya ya kitaifa dhidi ya rushwa.GlobE Network,ambao ulianzishwa mwaka 2021,umelenga kuongeza ushirikiano na kubadilisha taarifa ,uzoefu na utaalamu kati ya mamlaka mbalimbali duniani katika kupambana na rushwa.TAKUKURU ilijiunga na mtandao huu mwaka 2022 na imekuwa ikishiriki kikamilifu katika shughuli zake.

Katika mkutano huu,Chalamila pia alipata Fursa ya kukutana na viongozi wa mamlaka  nyingine za kuzuia na kupambana na rushwa,zikiwemo National commission of Supervision (NCS) ya China Beijing,Independent Commission Against Corruption(ICAC)ya Hong Kong ,na National Prosecutions Authority (NPA)ya Afrika Kusini.Mazungumzo yao yalilenga kuimarisha ushirikiano katika maeneo ya mafunzo ya uchunguzi ,ufuatiliaji na urejeshaji wa mali,ushahidi wa kiuchunguzi (forensic evidence),intelijensia na utoaji wa rlimu kwa umma.Viongozi Hawa wamepongeza juhudi za TAKUKURU na kuahidi kuendeleza ushirikiano katika nyanja hizo muhimu.

Katika hatua nyingine,Mkurugenzi Mkuu Bw Chalamila alikutana na balozi wa Tanzania nchini China ,Mhe khamis Mussa Omar,kwa lengo la kujitambulisha na kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu mapambano dhidi ya rushwa.Balozi Omar alitumia fursa hiyo kuipongeza TAKUKURU kwa jitihada zake katika kuzuia na kupambana na rushwa na kuhimiza kuendelea kutumia fursa za ushirikiano zilizopo kati ya Tanzania na China kwa manufaa ya taifa 

Mkutano huu unaonesha dhamira ya dhati ya TAKUKURU katika kuhakikisha rushwa inadhibitiwa kwa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kujenga mifumo imara ya kisheria na kitaasisi .Kwa ushirikiano huu,Tanzania inatarajia kupiga hatua kubwa zaidi katika mapambano dhidi ya rushwa,hivyo kuleta uwazi na uwajibikaji zaidi katika uendeshaji wa shughuli za umma na sekta binafsi.



 

Comments

Popular posts from this blog

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MAENDELEO YA CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA