RAIS WA UTPC AFURAHISHWA NA UBUNIFU WALIOONESHA WAANDISHI WA HABARI

 Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania(UTPC)  Deogratius Nsokolo akiwa ameambatana na Wajumbe wa bodi ya UTPC wametembelea mabanda ya maonesho ya kazi wanazofanya wanachama  wa Umoja huo na kujionea namna ambavyo Waandishi wanafanya kazi za kihabari na kuibua changamoto kwenye jamii.

Nsokolo amefurahishwa na namna ambavyo Waandishi wamekuwa wabunifu katika maonesho hayo ambayo yamefanyika katika viwanja vya Ofisi ya UTPC jijini Dodoma.

Aidha Nsokolo amesema kupitia maonesho hayo Waandishi wameweza kuonesha shughuli za kiuchumi wanazozifanya na kujikita katika Habari za uchunguzi.

Kwa upande wa mwakilishi wa Shirika la Twaweza ambao wamejikita katika kufanya tafiti za Sauti za Waandishi wa Habari Bi.Jane Shussa amesema ili Vyombo vya  habari viweze kupiga hatua na kuweza kujitegemea ni Lazima wao waweze kubadilika na kuandika Habari zenye ukweli.

Naye,Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC Kenneth Simbaya amesema maonesho hayo yamekuwa na faida kubwa na kuahidi kuwa mwaka ujao kuyafanya kwa ukubwa zaidi.





Comments

Popular posts from this blog

WALIOFUKUA KABURI WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI RUKWA

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

ZIMAMOTO YATOA MAFUNZO KWA WATUMISHI RUKWA.