UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

 Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Deogratius Nsokolo amesema ili kusaidia kupunguza hali ya uhasama dhidi ya Waandishi wa Habari UTPC inaendelea kutumia Klabu za Waandishi wa Habari mikoani kuhamasisha na kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa Uhuru wa  vyombo vya Habari na jukumu la Waandishi wa Habari katika jamii. 

Nsokolo ameyasema hayo Leo Novemba 2,2023 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa siku ya Kimataifa ya kukomesha Uhalifu dhidi ya Waandishi wa Habari ulioandaliwa na UTPC na kufanyika kwa njia ya mtandao(Zoom).

Amesema maadhimisho hayo kwa mwaka 2023 yanalenga Kuongeza uelewa kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo Waandishi katika kutekeleza majukumu Yao,lakin pia kuonya juu ya kukithiri kwa vitendo vya kikatili na ukandamizaji dhidi ya Waandishi wa Habari.

Aidha akiongelea kujenga Mazingira salama kwa Waandishi wa Habari amewashukuru ubalozi wa Uswiss hapa Nchini Tanzania,kwa ufadhili wao katika mradi na Mkuu wa jeshi la polisi Nchini IGP Camilius Wambura,kwa kuendelea kushirikiana na UTPC katika kuhakikisha Usalama wa Waandishi wa Nchini unakuwepo na hivyo kuwawezesha kuendelea kutimiza jukumu la kikatiba kwa mujibu wa ibara ya 18 ya katika ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



Naye,Mkurugenzi wa UTPC Bw.Kenneth Simbaya amewataka Waandishi wa Habari kuyapa kipaumbele masuala yanayowahudu kwa kushiriki kikamilifu na kutoa maoni ili kujiimarisha na kuweza kusaidia jamii kikamilifu.


Comments

Popular posts from this blog

Watumishi Wa Umma Wilayani Kalambo Waungana Kuadhimisha Kumbukizi Ya Mashujaa Kwa Kufanya Usafi.

Dc Kalambo Ataka Walio Husika Kumuozesha Mwanafunzi Wa Darasa La Saba Kukamatwa

Mkurugenzi UTPC awataka Waandishi kuandika Habari za Usawa wa kijinsia ili kuleta mabadiliko Chanya katika jamii.