BALOZI WA SWEDEN NCHINI ATEMBELEA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI KILIMANJARO

 

Mwandishi wetu

Jana Agosti 5,2024 Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh.Charlotta Ozaki Macias ametembelea klabu ya waandishi wa Habari Kilimanjaro (MECKI) kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na klabu hiyo pamoja na kufanya mazungumzo na wanachama wa klabu hiyo.

Mh.Balozi pia ametaka kujua mchango wa MECKI kwa jamii katika kupaza sauti Ili kuibua Changamoto zilizopo kwenye jamii na namna klabu hiyo ilivyojipanga kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu 2025.

Pamoja na mambo mengine Mh.Balozi na wanachama hao wamejadiliana masuala mbalimbali ikiwemo uhuru wa Vyombo vya Habari na namna ya kuandika Habari za uchunguzi.

Aidha Mh. Charlotta ameambatana na timu kutoka Muungano wa klabu za waandishi wa Habari Tanzania (UTPC)iliyokuwa ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Kenneth Simbaya.




Comments

Popular posts from this blog

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MAENDELEO YA CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA