Posts

Showing posts from July, 2021

MKIRIKITI; MYAPUUZE MANENO YA WANAOPTOSHA JUU YA Uviko 19

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joseph Mkirikiti Ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa manispaa ya Sumbawanga kukamilisha majengo ya shule na Zahanatiyaliyo katika hatua za mwisho ili kuepusha msongamano madarasani na vituo vya Afya katika kipindi hiki cha kupambana na wimbi la tatu la Uviko 19 wakati akikagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika manispaa ya Sumbawanga .Aidha amewataka wanachi kupuuza watu wanaopotosha juu ya Uviko 19 na badala yake wazingatie Ushauri unaotolewa na wahudumu wa Afya na Serikali kwa ujumla.Imeandaliwa na Peter Helatano

WALIOFUKUA KABURI WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI RUKWA

  Jeshi la Polisi mkoani Rukwa linawashikilia watu watatu wote wakazi wa Kirando wilayani Nkasi kwa tuhuma ya kufukua kaburi la marehemu asiyefahamika jina lake na kukata kichwa chake kisha kwenda kukitelekeza kwenye kichanja cha kuanikia vyombo nje ya nyumba ya mkazi mmoja wa kijiji cha Kirando Mkoani Rukwa.  Regina Samwel   katika maelezo yake anadai aliamka kwenda uani lakini   anakutana na harufu kali isiyoyakawaida hivyo alirudi ndani kumwarifu mamake   aliyetoka nje   na kukuta kichwa cha binadamu kimehifadhiwa kwenye sufuria juu ya kichanja cha vyombo kilichopo nje ya nymba yao.   Katika uchunguzi wa awali wa Polisi katika eneo la Kirando walifanikiwa kumkamata mtu mmoja kutokana na mfanano wa nyayo zake zilizoonekana kwenye eneo la tukio na hata kwenye kaburi hilo, hali iliyowashangaza hata wakazi wa eneo hilo wakidai kuwa hawajawahi ona tukio la aina hiyo maisha mwao. Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa William Mwampaghale amesema licha ya ku...

TUJITOE TUJENGE SHULE YETU,KERO YA BARABARA ZA MITAA WENYEVITI ZIWEKENI WEZI ZITANBULIKE KWENYE MFUMO

Image
  Ni miezi kadhaa tangu Mh mnanka kuchaguliwa kwake na wananchi wa kata ya msuwa ili aiongoze kata hiyo na kufikia malengo huku changamoto mbalimbali kama vile shule,barabara na maji vikiwa vikwazo katika kata hiyo.Leo ni mkutano wake muhimu wa kueleza mpango kazi na mikakati ya kuhakikisha kata hiyo inakuwa na maendeleo swali kubwa kwa wananchi ni kuhusu ukarabati wa barabara za mitaa kwaani imekuwa kero kubwa kwa wananchi kata hiyo Mh. Mnanka anawaasa wenyekiti wa   mitaa kushugulikia barabara za mitaa yao ili ziingie kwenye mfumo   zitambuliwe na hatimaye kukarabatiwa Kero nyingine kubwa ni shule kwani watoto wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kufata masomo yao hali iliyopelekea   mh diwani kukaa na wananchi wake kuamua kuchangia ili waanze ujenzi wa shule,wananchi nao wameitikia wito na  kutoa  maoni yao juu ya ujenzi wa shule kuwa uendelee kwa kuchangia kila Kaya ili kuanza ujenzi wa vyumba vya madarasa.

KUELEKEA MCHEZO WA TZ PRISON NA BIASHARA UNITED...USHINDI LAZIMA

Image
 Kikosi cha Tanzania Prison kimejiandaa vizuri katika kuwakabili wahasimu wao Biashara United katika mchezo wao utakaochezwa katika dimba la Nelson Mandela mjini Sumbawanga. SHABANI KAZUMBA Kocha msaidizi wa club hiyo anasema kikosi chake kimajiandaa vikali kuhakikisha wanapata ushindi kwani wakikutana na timu yake pinzani huwa wanasumbuliwa wakiwa ugenini hivyo atatumia vyema nafasi yake ya Nymbani kuhakikisha anachukua pointi 3 muhimu kutoka kwa Biashara united....Imeandaliwa na PETER HELATANO