WAKULIMA WA TANZANIA WASHAURIWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA KISASA ILI KUKUZA MAZAO YA KILIMO

 

Takribani wakulima 40,000 kunufaika na mradi wa upimaji wa udongo kwa ajili ya shughuli za kilimo

Zaidi ya wakulima 10,000 kutoka mkoa wa Rukwa kunufaika na mradi huu



Wakulima wa Tanzania washauriwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kukuza mazao ya kilimo.

Kampuni ya OCP Afrika iliyo kinara katika uzalishaji wa mbolea ulimwenguni, yazindua rasmi awamu ya pili ya mradi wa tathmini ya udongo ili kutoa elimu kwa wakulima juu ya aina za udongo na mazao rafiki kulimwa katika mikoa husika.

Mei 21, 2021 wakulima pamoja na viongozi wa Serikali wanatarajiwa kujionea mapendekezo bora juu ya aina za mbolea kutokana na aina ya udongo uliopo. Wakulima watakutanishwa na wataalamu wakaoongeze ufanisi kwenye shughuli zao za kilimo.

OCP Afrika kupitia kampuni tanzu ya OCP Tanzania kwa ilizindua awamu ya kwanza mradi wa tathmini ya udogo mwaka 2019, na awamu hii ya pili ya mradi huo unatarajiwa kuhudumia wakulima na wadau wa kilimo wa mikoa ya Rukwa, Morogoro, Mbeya na Iringa kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Idara za Kilimo (taasisi ya utafiti wa kilimo (TARI) kituo cha Uyole), tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI). Kampuni ya OCP Tanzania inatoa ushauri nasaha kwa mkulima mmoja mmoja na mapendekezo yanayolenga kustawisha ukuaji wa mazao kama mahindi, mpunga, viazi pamoja na alizeti.

Mradi huu ni mwendelezo wa awamu ya kwanza iliyozinduliwa mwaka 2019 na kufikia wakulima na wadau wa kilimo 20,000 katika mikoa za Njombe na Songwe. Majibu ya utafiti wa udongo kwenye mikoa hii yameweka bayana kwamba ukiachia mbali upungufu wa madini ya Fosforas na Naitrojeni uliopo kwa kipindi kirefu, kuna upungufu pia wa madini ya Zinki, Salfa pamoja na Potasiamu.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo wa mradi wa awamu ya pili mjini Sumbawanga,Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya OCP Tanzania Dkt. Mshindo Msolla alisema, "OCP Tanzania ikishirikiana na Serikali imeandaa mchakato wa upimaji wa udongo kwa zaidi ya vijiji 100 ndani ya mkoa wa Rukwa. Lengo ni kuwaelimisha wakulima juu ya udongo wa eneo lao bila gharama zozote kwa wakulima hao. Majibu yatatolewa kwao pamoja na ushauri wa kitaalamu juu ya nini kifanyike ili kutunza ubora wa udongo wa kijiji husika kwa matokeo bora ya shughuli za kilimo. Katika kila kijiji zaidi ya wakulima 100 watafikiwa na kuelimishwa namna bora za kufanya kilimo kiwe cha mahindi, mpunga au alizeti kulingana na maeneo waliopo. Na kwa mradi huu tunazamia kufikia wakulima 10,000 kwa mkoa wa Rukwa pekee.

Mradi huu wa upimaji na tathmini ya udongo unatarajiwa kuendeshwa katika vijiji 400 na kuwafikia wakulima wapatao 40,000 kufikia mwisho wa mwaka 2021. Mradi huu pia unatarajiwa kutoa mapendekezo ya mbolea kwa wakulima wapatao 14,000 watakao wakilisha wakulima wenzao kutoka mashamba mbalimbali kwa kutumia njia rahisi za upimaji udongo na kupata matokeo sahihi.

"Ni jambo lenye ulazima, kwamba wakulima wetu wawe rafiki na teknolojia za kisasa zitakazowawezesha kuongeza uzalishaji wao, na hivyo kuondokana na umasikini. Mradi huu wa upimaji na tathmini ya udongo ni jambo la kipekee sana na hivyo tunahamamisha wakulima wote wawe sehemu ya mradi huu". Aliongeza Dkt. Msolla.

Tangu mwaka 2017 zaidi ya wakulima 390,000 wamenufaika na miradi ya upimaji na tathmini wa udongo kutoka nchi nane barani Afrika za Naijeria, Togo, Ghana, Guinea, Kenya, Burkina Faso, Cote D'Ivoire na Senegal na kwa namna ya kipekee Tanzania inaungana na nchi hizo kuwa moja wa nchi wanufaika wa mradi huo.

Mradi huu wa upimaji na tathmini unaratibiwa kwa ushirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya kilimo, Tawala za mikoa na Serikali za mitaa pamoja na Taasisi ya utafiti wa Kilimo (TARI) wataalamu wa maendeleo ya kilimo.

"Mradi wa upimaji na tathmini wa udongo unaoongozwa na OCP kwa sasa ni nyenzo madhubuti kwa wakulima utakaokua na msaada mkubwa kwa kuongeza kiwango cha uzalishaji mazao". Alihitimisha Dkt. Msolla.

Kuhusu OCP Afrika:

OCP Afrika ilianzishwa mwaka 2016 ikifanya kazi bega kwa bega na wakulima ili kuleta maendeleo ya Kilimo. Tunazalisha mbolea za aina mbalimbali zinazoendana na uhitaji wa mazao husika, na tunafanya kazi pamoja na washirika mbalimbali zikiwemo serikali za kitaifa, taasisi na mashirika binafsi ili kuwaunganisha wakulima na mahitaji yao, ufahamu na mallighafi ili waweze kufanikiwa. Tuna uelewa mkubwa juu ya ujitaji wa udongo wa Afrika na tumejiatiti kuipatia Afrika mbolea inayohitajika kwa wakati husika, mahala husika na kwa bei rafiki.

Ikiwa na makao makuu yake Morocco, kampuni ya OCP Afrika ni kampuni tanzu ya OCP Group vinara wa uzalishaji wambolea ulimwenguni yenye uzoefu wa miaka zaidi ya 100.

Kwa taarifa zaidi tembelea www.ocpgroup.ma

Kuhusu Taasisi ya utafiti wa kilimo (TARI)

Kwa mujibu wa serikali ya Tanzania, taasisi ya utafiti wa kilimo (TARI) iliundwa ili kutatua changamoto za upimaji udongo, sampuli pamoja na kutoa nasaha zitakazo imarisha ukuaji wa kilimo katika ngazi za vijiji, wilaya na mikoa. Kwa kushirikiana na kampuni ya OCP Afrika na serikali za mitaa.

Kazi kubwa ya mshirika huyu ni kuweka mabaya mapungufu yaliyopo kwenye virutubisho vya udongo na kupendekeza mbolea bora kulingana na mapungufu hayo.

Kwa taarifa zaidi tembelea www.tari.go.tz

Maulizo kwa vyombo vya habari

OCP Tanzania LTD.

Bw.. Hillary Pato

Barua pepe:hd.pato@ocpafrica.com

Comments

Popular posts from this blog

Watumishi Wa Umma Wilayani Kalambo Waungana Kuadhimisha Kumbukizi Ya Mashujaa Kwa Kufanya Usafi.

Dc Kalambo Ataka Walio Husika Kumuozesha Mwanafunzi Wa Darasa La Saba Kukamatwa

Mkurugenzi UTPC awataka Waandishi kuandika Habari za Usawa wa kijinsia ili kuleta mabadiliko Chanya katika jamii.