Posts
Showing posts from August, 2022
PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA MAPOKEZI YA RC SENDIGA MKOANI RUKWA
- Get link
- X
- Other Apps
RC SENDIGA: TUTAFANYA MAPINDUZI YA KILIMO RUKWA
- Get link
- X
- Other Apps
RC SENDIGA: TUTAFANYA MAPINDUZI YA KILIMO RUKWA Na. OMM Rukwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga amesema anatamani kuona mkoa wa Rukwa ukifanya mapinduzi makubwa katika sekta ya kilimo kiwe cha kibiashara na kukuza uchumi wa wananchi. Ili kufanikisha hilo amewataka wataalam wa kilimo katika halmashauri zote nne za Rukwa kuja na mikakati ya kufanya kilimo kichangie zaidi katika kukuza pato la wananchi na kuongeza uhakika wa chakula. Mkuu huyo wa Mkoa amesema hayo jana mjini Sumbawanga (10 Agosti, 2022) wakati wa hafla rasmi ya makabidhiano ya ofisi toka kwa mtangulizi wake Joseph Mkirikiti kufuatia Rais Samia Suluhu Hassan kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. “Natamani kuiona Rukwa ikifanya mapinduzi makubwa katika kilimo. Maafisa kilimo na ugani jitahidini kuwa na mipango mizuri ili kilimo chetu kiwe cha kibiashara na kuhusisha vijana wengi “alisema Sendiga. Sendiga aliongeza kusema mkoa lazima uwe na mkakati wa kufanya vijana wengi kurudi vijijini ili kufanya ...
WAFANYABIASHARA MKOANI RUKWA WAELEZA SABABU ZA KUENDELEA KUPANDA KWA BEI YA BIDHAA
- Get link
- X
- Other Apps
WAFANYABIASHARA MKOANI RUKWA WAELEZA SABABU ZA KUENDELEA KUPANDA KWA BEI YA BIDHAA RUKWA-SUMBAWANGA.na Peter Helatano Wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi Mkoani Rukwa wamesema wingi wa Tozo zinazotozwa na serikali na mamlaka zake sanjari na kupanda kwa gharama za usafirishaji wa bidhaa za ujenzi ndicho chanzo cha kupanda kwa bei kubwa ya bidhaa hizo. Hayo yemeelezwa na wafanyabiashara mjini Sumbawanga sababu zinazowapelekea kupandisha bei ya bidhaa ya vifaa vya ujenzi huku wananchi wakilalamika kwa maumivu waanayoyapata na Kuiomba serikali kuondoa baadhi ya tozo zinazokuwa kikwazo katika biashara ya vifaa vya ujenzi. Aidha kupanda kwa bei ya mafuta kumepelekea kuongezeka kwa gharama za usafirishaji hali inayoongeza bidhaa za ujenzi kupanda bei ili kuwasaidia wauzaji kupata faida na kuweza kumudu gharama za usafirishaji wa bidhaa kutoka nje na ndani.
WANANCHI WATAKA ZAO LA KAHAWA KUPEWA KIPAUMBELE
- Get link
- X
- Other Apps
WAKULIMA WATAKA ZAO LA KAHAWA KUPEWA KIPAUMBELE ZAIDI KALAMBO-RUKWA. Na Peter Helatano Wakulima wa zao la Kahawa wilayani Kalambo Mkoani Rukwa wameiomba Serikali kuwekeza taika kilimo cha zao la kahawa ili kuwawezesha kuondokana na kilimo cha mazoea na kufanya zao hilo kuwa kubwa na la biashara kwa kutoa Ruzuku na mbegu za kutosha ili wazalishe zao hilo kwa tija. Wakiongea katika nyakati tofauti tofauti wakulima wilayani humo wamesema Serikali haina budi kuwekeza zaidi katika zao la kahawa kwa kutenga bajeti kila mwaka kwa ajili uendeshaji wa zao hilo ambalo litasaidia kujikwamua kiuchumi kutokana na soko lake kuwa kubwa nal auwazi duniani. Akiongea na wakulima wilayani humo kaimu Afisa kilimo wilayani Kalmbo Elieza Stephen, amesema katika msimu wa kilimo wa mwaka 2021/2022 zaidi ya hekali 30 zimepandwa na Serikali kutoa ruzuku.