WANANCHI WATAKA ZAO LA KAHAWA KUPEWA KIPAUMBELE



 

WAKULIMA WATAKA ZAO LA KAHAWA KUPEWA KIPAUMBELE ZAIDI

KALAMBO-RUKWA.

Na Peter Helatano

Wakulima wa zao la Kahawa wilayani Kalambo Mkoani Rukwa wameiomba Serikali kuwekeza taika kilimo cha zao la kahawa ili kuwawezesha kuondokana na kilimo cha mazoea na kufanya zao hilo kuwa kubwa na la biashara kwa kutoa Ruzuku na mbegu za kutosha ili wazalishe zao hilo kwa tija.

Wakiongea katika nyakati tofauti tofauti wakulima wilayani humo wamesema Serikali haina budi kuwekeza zaidi katika zao la kahawa kwa kutenga bajeti kila mwaka kwa ajili uendeshaji wa zao hilo ambalo litasaidia kujikwamua kiuchumi kutokana na soko lake kuwa kubwa nal auwazi duniani.

Akiongea na wakulima wilayani humo kaimu Afisa kilimo wilayani Kalmbo Elieza Stephen, amesema katika msimu wa kilimo wa mwaka 2021/2022 zaidi ya hekali 30 zimepandwa na Serikali kutoa ruzuku.

Comments

Popular posts from this blog

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MAENDELEO YA CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA