WAFANYABIASHARA MKOANI RUKWA WAELEZA SABABU ZA KUENDELEA KUPANDA KWA BEI YA BIDHAA
WAFANYABIASHARA MKOANI RUKWA WAELEZA
SABABU ZA KUENDELEA KUPANDA KWA BEI YA BIDHAA
RUKWA-SUMBAWANGA.na Peter Helatano
Wafanyabiashara wa vifaa vya
ujenzi Mkoani Rukwa wamesema wingi wa Tozo zinazotozwa na
serikali na mamlaka zake sanjari na kupanda kwa gharama za usafirishaji wa
bidhaa za ujenzi ndicho chanzo cha kupanda kwa bei kubwa ya bidhaa hizo.
Hayo
yemeelezwa na wafanyabiashara mjini
Sumbawanga sababu zinazowapelekea kupandisha bei ya bidhaa ya vifaa vya ujenzi
huku wananchi wakilalamika kwa maumivu waanayoyapata na Kuiomba serikali kuondoa baadhi ya tozo zinazokuwa kikwazo
katika biashara ya vifaa vya ujenzi.
Aidha
kupanda kwa bei ya mafuta kumepelekea kuongezeka kwa gharama za usafirishaji hali
inayoongeza bidhaa za ujenzi kupanda bei ili kuwasaidia wauzaji kupata faida na
kuweza kumudu gharama za usafirishaji wa bidhaa kutoka nje na ndani.
Comments
Post a Comment