Posts

Showing posts from April, 2021

Muungano Tanganyika na Zanzibar

Leo Aprili 26, 2021 nchi yetu inaadhimisha miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa na Waasisi wa Taifa letu Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Abeid Karume ambao ulizaa Taifa moja la Tanzania. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinawatakia Watanzania wote Sherehe njema za Sikukuu hii ya Muungano huku tukiendelea kulinda tunu muhimu za Taifa letu ambazo ni amani, umoja, upendo na mshikamano. #Zegehalilali #Achakaziiendelee #TunaimaninaSamia

JEREMIAH MGUNDA KUIPAISHA TZ PRISON DHIDI YA RUVU SHOOTING

Image
Goli la Jeremiah Mgunda limeipatia timu ya Tz Prison pointi tatu kwa ushindi wao wao wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika uwanja wa Nelson Mandela stadium Sumbawanga Katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.

KITUO CHA UWEZESHAJI WANACHI KIUCHUMI KUZINDULIWA RASMI SUMBAWANGA

 Wananchi Kupata fursa ya kujifunza uchumi,biashara,mikopo,kampuni na viwanda kupitia kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi kilichozinduliwa Aprili 23,2021 katika viunga vya bustani Uwanja wa Nelson Mandela Sumbawanga. Ikiwa ni kutii Agizo na maelekezo yaliyotolewa na Waziri mkuu Mh.Kasim Majaliwa mwaka 2018 akiwa ziara Kahama Alizitaka halmashauri zote nchini kuanzisha kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi.Kutokana na agizo hilo halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga Wamechukua hatua mathubuti ili kutekeleza jitihada na shughuli za serikali kuanzisha kituo hiki cha uwezeshaji wananchi kiuchumi kushirikiana na wadau kufanikisha malengo ya kituo.
Image
 JUKWAA LA UCHUMI KUZINDULIWA HIVI KARIBUNI Wananchi kupata fursa ya kujifunza Biashara,uchumi,mikopo,kampuni na viwanda Kupia kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi kinachozinduliwa Aprili 23,2021 katika viunga vya bustani Uwanja wa Nelson Mandela Sumbawanga mjini.Hivyo ni muda sasa wananchi pamoja na wadau wengine wa maendeleo kujitokeza katika viunga hivyo. “Frank Maten”