KITUO CHA UWEZESHAJI WANACHI KIUCHUMI KUZINDULIWA RASMI SUMBAWANGA
Wananchi Kupata fursa ya kujifunza uchumi,biashara,mikopo,kampuni na viwanda kupitia kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi kilichozinduliwa Aprili 23,2021 katika viunga vya bustani Uwanja wa Nelson Mandela Sumbawanga. Ikiwa ni kutii Agizo na maelekezo yaliyotolewa na Waziri mkuu Mh.Kasim Majaliwa mwaka 2018 akiwa ziara Kahama Alizitaka halmashauri zote nchini kuanzisha kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi.Kutokana na agizo hilo halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga Wamechukua hatua mathubuti ili kutekeleza jitihada na shughuli za serikali kuanzisha kituo hiki cha uwezeshaji wananchi kiuchumi kushirikiana na wadau kufanikisha malengo ya kituo.
Comments
Post a Comment