Posts

Showing posts from April, 2020

Mwakilishi wa Ubalozi wa Pakistani, Muhammad Saleem ameipongeza serikali ya Tanzania kwa hatua ilizochukua kudhibiti #COVIDー19

Image
Mwakilishi wa Ubalozi wa Pakistani, Muhammad Saleem ameipongeza serikali ya Tanzania kwa hatua ilizochukua kudhibiti #COVIDー19 na kuongeza kuwa, tangu ugonjwa huo ulipoingia nchini kasi ya maambukizi ni ndogo ukilinganisha na nchi nyingine, sababu ya hatua thabiti za serikali.

Mauritania haijarekodi kisa kingine cha coronavirus

Image
Mauritania haijarekodi kisa kingine cha coronavirus, siku 2 baada ya mgonjwa wa mwisho kupona. Nchi hiyo ilikuwa na wagonjwa 7, ambapo 6 wamepona & mmoja amefariki. Wagonjwa waliopona wataendelea kutengwa kwa siku 14. Nchi hiyo iliripoti kisa cha kwanza Machi 13, 2020.

Serikali imekubali maombi ya familia ya mwendazake Askofu Dkt. Getrude Rwakatare

Image
Serikali imekubali maombi ya familia ya Mwendazake Askofu Dkt. Getrude Rwakatare kwamba mama yao azikwe Aprili 23, 2020 katika eneo la Kanisani la Mlima wa Moto. Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema serikali ndiyo itakayosimamia mazishi hayo ambayo washiriki wake hawatozidi 10.