WANANCHI WAOMBA ULINZI WA JESHI MWAMBAO MWA ZIWA TANGANYIKA.
WANANCHI WAOMBA ULINZI WA JESHI MWAMBAO MWA ZIWA TANGANYIKA.
Na Peter Helatano
Wakazi wa Vijiji vya Kata za KIZUMBI, WAMPEMBE,
KIRANDO, na KABWE Katika wilaya ya NKANSI, Mkoani Rukwa, wameiomba Serikali
Ulinzi kutokana na wimbi la Ujambazi kukithiri mwambao mwa ziwa Tanganyika
upande wa Vijiji hivyo.
Katika Mkutano wa hadhara uliofanhyika katika
Kijiji cha LYAPINDA, Kata ya KIZUMBI, wananchi wamemwambia Mkuu wa mkoa kuwa
watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wamekuwa wakipora Mali na vifaa vyao vya Uvuvi, na kusababisha hofu kwa
wananchi wa vijiji kuzunguka ziwa Tanganyika upande wa mkoa wa Rukwa.
Katika mkutano wa hadhara wa wananchi wa Vijiji
vya Kata ya Kizumbi na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa QUEEN SENDIGA. Mkutano huo wa
wananchi umelenga kueleza kero zao zinazowakabili za kukosekana kwa usalama
mwambao mwa ziwa Tanganyika. Wananchi wakaenda mbali zaidi kuomba kikosi cha
Jeshi la Wananchi wa Tanzani-JWTZ ili kukomesha matukio ya ujambazi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa QUEEN SENDIGA
amewahakikishia wananchi wa Kata nne zinazokabiliwa na matukio ya ujambazi mara
kwa mara.
Aidha Mkuu wa mkoa QUEEN SENDIGA ameigeukia idara
ya uhamiaji kuwajibika huku mpakani lakini pia kuwanyoshea kidole wamiliki wa
nyumba za kulala wageni.
Comments
Post a Comment