WANANCHI WAOMBA ULINZI WA JESHI MWAMBAO MWA ZIWA TANGANYIKA. Na Peter Helatano Wakazi wa Vijiji vya Kata za KIZUMBI, WAMPEMBE, KIRANDO, na KABWE Katika wilaya ya NKANSI, Mkoani Rukwa, wameiomba Serikali Ulinzi kutokana na wimbi la Ujambazi kukithiri mwambao mwa ziwa Tanganyika upande wa Vijiji hivyo. Katika Mkutano wa hadhara uliofanhyika katika Kijiji cha LYAPINDA, Kata ya KIZUMBI, wananchi wamemwambia Mkuu wa mkoa kuwa watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wamekuwa wakipora Mali na vifaa vyao vya Uvuvi, na kusababisha hofu kwa wananchi wa vijiji kuzunguka ziwa Tanganyika upande wa mkoa wa Rukwa. Katika mkutano wa hadhara wa wananchi wa Vijiji vya Kata ya Kizumbi na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa QUEEN SENDIGA. Mkutano huo wa wananchi umelenga kueleza kero zao zinazowakabili za kukosekana kwa usalama mwambao mwa ziwa Tanganyika. Wananchi wakaenda mbali zaidi kuomba kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzani-JWTZ ili kukomesha matukio ya ujambazi. Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ...