Posts

Showing posts from November, 2022

UVCCM MKOA WA RUKWA WAKUTANA

Image
 UVCCM MKOA WA RUKWA Leo asubuh tarehe 29/11/2022 Mwenyekit wa uvccm mkoa wa Rukwa ndugu Albert kipele amekutana na Makamu  Mwenyekit wa uvccm Taifa Bi,Rehema Sombi na kufanya naye Mazungumzo juu ya agenda za vijana Mkoani Rukwa  Mazungumzo hayo yalifanyika hotel ya Moreno Dodoma . mwenyekit alikuwa ameambatana na katbu wa uvccm wilaya ya kilosa,ukumbuke katibu wa uvccm wilaya ya kilosa ana vinasaba vya maendeleo na mkoa wa Rukwa Imetolewa na idara ya hamasa na chipukizi mkoa wa Rukwa  Makarius Kayumbi

Bashe akemea vikali wakulima wanaouza namba za

Image
 *Bashe akemea vikali wakulima wanaouza namba za siri* Waziri wa Kilimo Hussein Bashe leo tarehe 22.11.2022 amewakemea vikali wakulima wanaowauzia wafanyabiashara namba zao za siri kwa ajili ya kupata mbolea za ruzuku kwa njia za udanganyifu. Mhe.Bashe alizungumza hayo wilayani Kondoa  alipopewa nafasi na Mh Rais Samia Hassan Suluhu akiwa ziarani kuelekea Mkoani Manyara.  Waziri Bashe amesema wakati serikali ya Awamu ya  Sita inafanya kila jitihada kuwapunguzia  wakulima  gharama ya mbolea,  baadhi yao  wanahujumu jitihada hizo. Akitoa mfano Waziri huyo wa kilimo amesema wakulima wapatao 20 mkoani Kigoma wamekamatwa kwa tuhuma za  kuwauzia wafanyabiashara wa mbolea namba zao za siri kwa ajili kupata mbolea za ruzuku. "Napenda kuwafahanisha wakulima wote nchini kuwa mfumo tunaotumia kutoa mbolea za ruzuku ni wa kidigitali,  hivyo chochote kinachofanyika katika mfumo huo tunakifahamu", alisema Bashe. Amewaonya wote watakaojihusisha na vite...