VYOMBO VYA HABARI TOENI ELIMU KUTOKOMEZA UKATILI
Na Franco Nkyandwale-Sumbawanga.
TOENI ELIMU YA WIMBI LA UKATILI
Mkaguzi msaidi wa jeshi la polisi Wilaya ya Sumbawanga Winnie Dilli Amevitaka vyombo vya habari Mkoani Rukwa kuhakikisha wanatoa elimu juu ya Vitendo vya ukatili vinavyotokea kwa Jamii kama vile tabia za baadhi ya watu kuwalawiti watoto,Ukatili wa kijinsia,Masuala ya ndoa na migogoro mingine inayoweza kupelekea Vitendo vya ukatili.
Ameyasema hayo leo Katika maadhimisho ya vyombo vya habari klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Rukwa ambayo yamewakutanisha wadau mbalimbali Kutoka taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali ili kijadiki kwa pamoja Mambo muhimu Katika kuhabarishana na kuutangaza Mkoa wa Rukwa kupitia vyombo vya habari ikiwa Ni pamoja na kuweka wazi fursa za Mkoa wa Rukwa na kuzitangaza.
Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Rukwa Ndugu Nswima Enrest amewataka waandishi wa habari kujifunza zaidi kuhusu uandishi wa habari kidigitali ili kuendana na kasi ya maendeleo ya teknolojia na kufanya kazi zao kwa weredi, Aidha amewataka kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa kuzingatia kanuni na taratibu muhimu za kuzingatia katika upatikanaji na utoaji wa taarifaa.
Enrest amesema Teknolojia inakuwa kwa kasi zaidi hivyo ni vyema waandishi wa habari kujifunza ujuzi wa kuhakikisha wanafanya kazi zao bila kuingilia na watu wengine kama vile wadukuzi,Kupotea kwa data,Kujifunza sheria za makosa ya kimtandao,na Kupakua taarifa.
Aidha amewataka kuzingatia maudhui yaliyo sahihi katika utoaji wa taarifa ili kuhakikisha taarifa wanazotoa zinakuwa na ukweli na weredi na kuijenga jamii nzuri.
Maadhimisho ya Uhuru wa vyombo vya Habari klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Rukwa yamefanyika leo tarehe 16.05.2022 yakiwa na kauli mbiu ya '' Uandisi wa Habari na Changamoto za Kidigitali''.Publishe by Peter Helatano from Android Phone.
Comments
Post a Comment