RUWASA YATUMIA BILIONI 16 KUKAMILISHA MIRADI 39 YA MAJI RUKWA
RUWASA YATUMIA BILIONI 16 KUKAMILISHA MIRADI 39 YA MAJI RUKWA
Na OMM Rukwa
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Joseph Mkirikiti amepongeza Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini
(RUWASA) Mkoa wa Rukwa kwa kufanikiwa kutekeleza miradi 39 ya maji yenye
gharama ya shilingi Bilioni 16.6 katika mwaka wa fedha 2021/2022 kwenye mkoa wa
Rukwa ikiwa ni juhudi za kumtua mama ndookichwani.
Mkirikiti amesema hayo leo
(11 Aprili 2022) mjini Sumbawanga wakati akiongea kikao cha wadau wa maji
ulioratibiwa na RUWASA mkoani huo ukiwa na lengo la kuwafahamisha wadau hatua
zilizofikiwa kwenye utekelezaji bajeti na mipango ya kufikisha huduma za maji
vijijini.
Mkuu huyo wa Mkoa alitaja mafanikio mengine ya
RUWASA kuwa ni pamoja na huduma za upatikanaji maji kuongezeka kufikia asilimia
64 vijijini na mjini imefikia asilimia 86 kutokana na kukamilika kwa miradi
hiyo 39 kati ya miradi 99 yenye thamni ya shilingi Bilioni 25.5 iliyosainiwa
mwaka 2021/22 .
“Niwapongeze RUWASA kwa
usimamizi mzuri wa miradi hii ya maji, hatua hii inasaidia wananchi kupata maji
safi na salama na kuboresha afya hivyo kuwafanya wananchi waendelee kushiriki
vema kwenye utekelezaji shughuli za maendeleo” alisema Mkirikiti
Mkirikiti alibainisha kuwa
pamoja na jitihada za serikali kutoa fedha kwa miradi ya maji bado kuna
changamoto ya uharibifu wa mazingira hususan vyanzo vya maji ikiwemo shughuli
za kilimo ndani ya mita Sitini ya maziwa, mito na mabwawa .
“ Kama kuna fedha imeletwa
lazima uhakikishe mradi huo unakamilika , hilo ndio lengo la Rais Samia Suluhu
Hassan . Katika hili sihitaji kuona hadithi toka kwa watendaji ndani ya Rukwa”
alisisitiza Mkirikiti.
Kwa upande wake Meneja wa
RUWASA Mkoa wa Rukwa Mhandisi Boaz Pius alisema lengo la kikao hicho ni kuwaeleza
wadau kuhusu juhudi zinazofanya na Wizara ya Maji katika kuondoa kero ya
ukosefu wa maji vijijini.
Mhandisi Boaz aliongeza
kusema RUWASA inaandaa mikakati kwa kuunganisha vyombo vya watumie maji kote
vijijini ili kuwa na vyombo vichachevenye wataalam waliobobea ili wasimamie
utoaji huduma badala ya kuwa na idadi kubwa ya vyombo hatua inayoongeza gharama
za uendeshaji.
Akitoa mada kuhusu
michango wa Vyombo vya Watumia Maji ngazi ya Jamii (CBWSOS) Afisa Maendeleo ya
Jamii RUWASA NanyariLona alisema kiasi cha shilingi 168,423,720 zimekusanywa na
vyombo ambapo kati ya hizo shilingi 127,033,162 zilirudishwa kwenda kuendesha
vyombo na matengenezo ya miundombinu ya maji.
Lona alieleza pia
mafanikio mengine ni kuwepo kwa mwamko wa jamii kuingiza maji majumbani ambapo
asimilia 45 ya kaya vijiji zimeunganisha huduma hiyo pia ajira 101 zimepatikana
kati hizo mafundiwapo 60 na wahasibu 41.
Kwa upande wake Mwakilishi
wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa EnosBudodiambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Wazazi Mkoa aliwapongeza RUWASA kwa mafanikio waliyoyapata ambayo ni ishara
nzuri kuwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM inatekelezwa.
Kikao hicho cha wadau wa
maji kimehudhuriwa na Wakuu wa Wilaya, Wajumbe wa Kamati ya Usalama Mkoa,
wahandisi wa RUWASA, SUWASA,Viongozi wa CCM toka wilaya zote, wakurugenzi na
wenyeviti wa halmashauri za Sumbawanga, Nkasi na Kalambo .
Mwisho.
Imewekwa na Peter Helatano
Comments
Post a Comment