WAGOMBANIA KUZIKA MWILI WA MAREHE,WAKILI ATOA UFAFANUZI KISHERIA


Baada ya familia mbili kugombania mwili wa marehemu na kuzua taharuki mjini Sumbawanga mkoani Rukwa huku Kila mtu akidai yeye ndio mwenye haki ya kuzika.

Wakili James Lubusi ametoa ufafanuzi juu ya Nani mwenye haki kisheria kuzika mwili wa marehemu,Lakini pia maetoa ushauri kwa wanajamii kuwa na utaratibu wa Kiandika Wosia ili kuepuka migogoroa mbalimbali katika ukoo au Familia.

Hapo awali mwezi januari,2022 ulitokea msiba ambao ulileta mgogoro kwa wanafamilia baada ya kuwa marehemu alikuwa ameoa wake wawili(Bi mkubwa na Bi mdogo) na kuzaa watoto lakini Alifanikiwa kufunga ndoa na Bibi mdogo.

Kwa Nini msiba ulileta mgogoro? Ni baada ya Bi mkubwa kudai yeye ndio was Kwanza kuwai kuolewa na marehemu bila kujali kuwa marehemu alifunga ndoa na Bi mdogo,Hali hiyo ilileta mvutano lakini pande zote mbili waliweka msiba na Kila mmoja alinunua jeneza kujiandaa kuhifadhi mwili wa marehemu.

Baadaya ya uamuzi wa mahakama kutenda haki badi ilibidi mwili uzikwe kwa mke wa ndoa na kwa kuwa familia hizi mbili ziliandaa makabuli kwa Mila za kifipa ilibidi kaburi moja lilizikwa mgomba kwani tayari lilikuwa limechimbwa.

 

Comments

Popular posts from this blog

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MAENDELEO YA CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA