NFRA YANUNUA TANI 4,600 ZA MAHINDI YA WAKULIMA RUKWA
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) imefanikiwa kununua tani 4,600 za mahindi zenye thamani ya Shilingi Bilioni Mbili na Milioni Mia tatu ( 2,300,000,000) toka kwa wakulima kati ya lengo la tani 5,000 zilizopangwa awamu ya kwanza kufikia Agosti 31, mwaka huu. Hayo yamebainishwa leo (01.09.2021) wakati Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Milton Lupa alipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti ofisini kwake Sumbawanga akiwa katika ziara ya kukagua zoezi la ununuzi wa mahindi Meupe linaloendelea katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.