NAMNA MRADI WA ELIMU JUMUISHI UNAVYOKUWA KWA JAMII
Mradi wa
elimu jumuishi Sumbawanga umekuwa na matokeo chanya kwa jamii,wanajamii
wamekuwa na uelewa mapana juu ya kuishi na watoto wenye mahitaji maalumu,namna
ya kuwahudumia na kuzingatia miundombinu itakayokuwa rafiki kwa watoto wawapo
nyumbani au shuleni pia. Lakini changamoto ni kwa baadhi ya shule kutotunza
miundombinu inayoboreshwa na mradi huu. Hivyo sisi kama wanajamii tuamke na
kuthamini msaada tunaopatiwa lakini pia kujitoa katika uchangiaji kwa watu
wenye mahitaji maalumu. Mradi huu unalenga kuwasaidia watu wenye mahitaji
maalumu ikiwa ni pamoja na kuwasaidia vifaa saidizi mradi ambao unasimamiwa na
ERICK KAMKONO ambao unaratibiwa na kanisa la FPCT na ICD Kwa hapa Tanzania.
Comments
Post a Comment