DK.MZINDAKAYA ALITOA MAELEKEZO HAYA AKIFA
Hayati Mpendwa mzee wetu Dk. Chrisant Mzindakaya mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania aliyefariki katika hospitali ya Mhimbili jijini Dar es salaam alikokuwa akitibiwa anatajarajiwa kuzikwa Alhamisi Juni 12,2021 mida ya saa 9 Alasiri. Msemaji wa familia Frank Mzindakaya amesema Mzindakaya kabla hajafariki alitoa maelekezo ywa mahali pa kuzikiwa akifa.Hivyo familia itatekeleza jambo hilo.Hayati mzee wetu Dk. Mzindakaya anashikilia rekodi ya kuwa kiongozi aliyedumu katika uongozi kwa mda mrefu rekodi ambayo bado haijavunjwa na mtu yoyote hapa nchini kwa takribani miaka 40.Pumzika kwa amani mzee wetu tutaenzi mema na ushauri wako katika kulijenga Taifa letu la Tanzania.Imeandaliwa na Peter Helatano