Mchango wa vyombo vya habari katika uchumi.
Sekta ya Habari imekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta za Uchumi za Mkoa (Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Biashara, Maliasili na Ushirika). Wanahabari wamekuwa wakitoa ushirikiano kwa kushiriki katika matukio na ziara mbalimbali za viongozi wa Kitaifa, Mkoa na Wilaya katika mkoa wetu na kurusha au kuandika katika vyombo vya habari (Redio, Runinga na Magazeti)
Vituo vya redio binafsi vya ndani ya mkoa viko mstari wa mbele kabisa katika kuchangia maendeleo ya sekta za uchumi za Mkoa kwa kujitolea muda hewani wa kurusha matangazo mbalimbali kufikisha elimu na utaalam kwa wananchi kwa kushirikiana na Wataalam wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Waandishi wa habari wamekuwa wakishiriki katika kutoa habari za mafunzo mbalimbali ya kilimo, mifugo, uvuvi n.k yanayofanyika katika mkoa mfano
Wamekuwa wakiandika makala mbalimbali za maendeleo ya uchumi ndani ya mkoa.
Kushiriki katika maadhimisho ya shughuli za kiuchumi yanayofanyika ndani ya mkoa mf.Siku za wakulima, Siku ya upandaji miti kimkoa, siku ya Mazingira na Makongamano ya uwekezaji
Comments
Post a Comment