MAFUNZO YA KUONGEZA UELEWA NA KUPUNGUZA UNYANYAPAA KWA JAMII NA WAHUDUMU WA AFYA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA WA WATU WENYE ULEMAVU.
.Shilikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania [ SHIVYAWATA]
Wameiomba serikali kuwepo haja ya kutoa
elimu kwa watoa huduma za Afya ili kuwahudumia kwa ustadi watu wenye ulemavu. Huduma za Afya kwa watu wenye ulemavu nchini Tanzania bado zinakabiliwa
na changamoto licha ya sera na sheria za nchi kusema kuwa kundi hili lipatiwe
bure matibabu ikiwemo kupewa kipaumbele. Baadhi ya changamoto wanazokutana nazo
watu wenye ulemavu katika kupata huduma za afya ni pamoja na;
•
Miundo mbinu isiyo rafiki katika
vituo vya kutolea huduma za afya mfano; vyoo, njia maalumu kwa ajili ya
walemavu. Pia baadhi ya watu wenye ulemavu kukosa vifaa saidizi kama vile wheel
chairs hivyo kuwa hatarini kupata maambukizi ya magonjwa wanapokuwa katika
vituo vya kupatia huduma za afya
•
Lugha (Mawasiliano) hasa kwa watu
wenye ulemavu wa kusikia (uziwi)na kutoongea hivyo kupelekea changamoto katika
kuwasiliana na watoa huduma kwani wengi hawajui lugha ya alama. Pia elimu ya
afya inayotolewa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kutowafikia ipasavyo
watu wenye ulemevu mfano watu wenye ulemavu wa kuona
Comments
Post a Comment