Being,China -Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU)inashiriki kongamano la 5 la kimataifa la mashirikiano katika mapambano dhidi ya rushwa,linaloendelea jijini Beijing China. Kongamano hili limewakutanisha mamlaka 219 kutoka nchi 121 duniani,likilenga kubafilishana uzoefu na utaalamu katika jukumu la kuzuia na kupambana na rushwa Kongamano hili la siku Tano limejumuisha warsha ya viongozi wa mamlaka za kuzuia na kupambana na rushwa(high level Forum),ambapo Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU ,Bw.Crispin Francis Chalamila,amewasilisha mada kuhusu "mfumo wa Sheria wa Tanzania katika mapambano dhidi ya rushwa"katika mada yake Bw.Chalamila ameeleza jinsi ambavyo serikali ya Tanzania imekuwa ikijipambanua katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kuimarisha mifumo ya Sheria na ya kitaasisi.Alibainisha uanzishwaji wa divisheni ya mahakama kuu inayoshughulikia masuala ya rushwa na uhujumu uchumi kuwa ni hatua muhimu katika kuhakikisha uwajibikaji na utawala Bora. TAKUKURU...
Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Deogratius Nsokolo amesema ili kusaidia kupunguza hali ya uhasama dhidi ya Waandishi wa Habari UTPC inaendelea kutumia Klabu za Waandishi wa Habari mikoani kuhamasisha na kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa Uhuru wa vyombo vya Habari na jukumu la Waandishi wa Habari katika jamii. Nsokolo ameyasema hayo Leo Novemba 2,2023 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa siku ya Kimataifa ya kukomesha Uhalifu dhidi ya Waandishi wa Habari ulioandaliwa na UTPC na kufanyika kwa njia ya mtandao(Zoom). Amesema maadhimisho hayo kwa mwaka 2023 yanalenga Kuongeza uelewa kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo Waandishi katika kutekeleza majukumu Yao,lakin pia kuonya juu ya kukithiri kwa vitendo vya kikatili na ukandamizaji dhidi ya Waandishi wa Habari. Aidha akiongelea kujenga Mazingira salama kwa Waandishi wa Habari amewashukuru ubalozi wa Uswiss hapa Nchini Tanzania,kwa ufadhili wao katika mradi na Mkuu wa jeshi la polisi Nchini IG...
Comments
Post a Comment