RUKWA

Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Rukwa Mh.Irene Ndyamkama ameanza ziara yake na kukabidhi mradi wa UWT ambao ni viti 100 vitakavyosaidia kukodisha na kuwaingizia kipato wanachama wa UWT , sambamba na hilo ameahidi  kuwalipia Bima ya Afya iliyoboreshwa CHF kwa mwaka mmoja,Ametoa mafunzo ya ujasiliamali na wakufunzi kutoka SIDO kwa lengo la kuwainua wajasiriamali.Mafunzo haya yamehusisha wajumbe mbalimbali kutoka katika kata 9 zilizopo manispaa ya Sumbawanga. Naye msemaji wa Bima iliyoboreshwa CHF Dr. Joseph Ngwale  kutoka kiyuo cha Afya Mazwi amezungumzia umuhimu wa Bima hiyo na kuwaasa watu kujitokeza kwa wingi kuweza kupata huduma za afya kwa urahisi pale tu unapohisi afya kuteteleka. Kwa upande wa wanawake waliopata Bima ya afya wameonesha nia ya dhati kuunga jitihada zinazofanywa na mbunge,pia kumpongeza kuwasaidia kupata Bima ya afya iliyoboreshwa.Mbunge wa viti maalumu Mh. Irene Ndyamkama anakutana na vikundi mbalimbali vya ujasiriamali vya akina mama na kuwaunga mkono katika jitihada zao kwa kuwapatia elimu ya ujasiriamali kutoka SIDO  Hali hii itasaidia kuinua uchumi katika kata mbalimbali. Mh Irene ameanza ziara yake ambayo atazunguka mkoa mzima wa Rukwa.




 

Comments

Popular posts from this blog

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MAENDELEO YA CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA