Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametoa maagizo kwa Manispaa ya Sumbawanga kukamilisha ujenzi wa shule ya msingi Mkuyuni ili kuepusha mlundikano na wanafunzi kutembea umbali kwenda shule ya Msingi King'ombe.
SERIKALI KUWEKA MIPAKA KULINDA VYANZO VYA MAJI
SERIKALI KUWEKA MIPAKA KULINDA VYANZO VYA MAJI Serikali Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa imeanza Uwekaji wa mipaka kati ya Pori la Akiba Lwafi na Kijiji cha Mtogolo kilichopo Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa ili Kulinda chanzo cha maji katika bwawa la Mfili amabalo ni tegemeo la maji Katika Wilaya ya Nkasi kutokana na bwawa hilo kukausha maji kutokana na shuguli za kibinadamu zinazodaiwa kufanyika pembezoni mwa bwawa hilo. Hayo yamejiri Katika zoezi la uhuishaji wa hifadhi ya msitu wa Lwafi ambopo Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Peter Lijualikali amewataka wananchi kuzingatia maelekezo ya Serikali ili kulinda vyanzo vya maji Wananchi Katika maeneo hayo wanadai kuishi mda mrefu huku kilio chao ni kuhakikisha wanapatiwa maeneo mengine kama walivyoahidiwa na Serikali
Comments
Post a Comment