Maelfu Ya Waumini Wajitokeza Kuombea Uchaguzi''kalambo.''
Na Baraka Lusajo. Rukwa Waamini pamoja na wachungaji kutoka madhehebu mbalimbali ya dini kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama wilayani Kalambo mkoani Rukwa, wameungana kuendesha kongamano la kumuomba mwenyezi Mungu ili uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu, uwe wa haki ili kuilinda amani na utulivu uliopo kwa lengo la kuivusha nchi ikiwa salama bila kumwaga damu. Makamu askofu wa kanisa la FPCT jimbo la Rukwa na katavi Andrea Mwakalinga amesema watumishi wa Mungu tunahitaji kamapeni safi bila ugomvi na kwamba kufanya fujo ni kukosa hekima ya kimungu. Amesema kwa kuwa wagombea wote wanatoka katika makanisa na misikiti yetu, Mashehe na Wachungaji tuta hakikisha tuna hubiri amani na utulivu kwenye mihadhara yetu. ‘’sisi t...